01 Apr 2020 Tukio Youth, education & environment

Huwezi kwenda kokote? Hapa kuna mawazo ya jinsi ya kushughulikia mazingira

Umelemewa? Hapa kuna mawazo ya jinsi ya kushughulikia mazingira

Je, umelemewa na kujitenga ili kusaidia kukabiliana na virusi vya korona? Je, uko katika karantini rasmi au umezuiwa kwenda popote? Je, umeanza kufanya kazi mpya kama "mwalimu wa nyumbani" kutokana na kufungwa kwa shule? Hapa kuna mambo unayoweza kufanya bila kutoka nyumbani- na mwanafunzi yeyote bila kujali umri anaweza kufurahia.

 

Tafakari kuhusu maji yaliyo ardhini ukiwa nyumbani kwako.

Anza safari ya kuogelea na kupiga mbizi kupitia kwa mtandao ukitazama matumbawe na bahari za kupendeza.

 

Hapa kuna mawazo ya shughuli zinazoweza kukuwezesha kutumia vitu vinavyoweza kupatikana nyumbani mwako. Miradi hii inaweza kusaidia watoto wa umri wowote kujifunza kuhusu tatizo la uchafuzi wa plastiki kwa njia ya ubunifu wanapokuwa wakipumzika.

 

Sasa, kuliko kipindi kingine chochote katika historia, ni wazi kuwa ni sharti tushirikiane kukabiliana na changamoto kuu zinazoikumba dunia. Kwa kutoa mafunzo na kujifundisha kutoka kwa vizazi vijavyo kuhusu changamoto za mazingira, kila mmoja anaweza kupiga hatua za kukabiliana na uchafuzi na kuwezesha kuwa na hatima endelevu.

 

Tufuatilie. Kuna uwezekana kuwa utatoa mipasho ya shughuli mpya na mawazo mapya katika majuma yajayo..