04 Apr 2019 Tukio Uchumi usiochafua mazingira

Kuiumba upya dunia

Leyla Acaroglu alikuwa na umri wa miaka 19 wakati wake wa kwanza kuhudhuria somo la kubuni michoro. Alisikia kitu ambacho kilibadili mtazamo wake kuhusu dunia milele.

Prof aliyemfundisha kubuni michoro alikuwa anafunza kuhusu nadhariatete ya Gaia: nadharia inayoshikilia kuwa kila kitu ulimwenguni kina uhusiano na kingine. Kama watu wa kubuni michoro, aliwasisitizia, kuna uwezekano kuwa siku moja watafanya maamuzi ambayo yatakuwa na athari kubwa mno kwa mazingira bila hata wao wenyewe kutambua.

"Niliketi pale huku nikiitazama picha ya tsunami na kuwaza 'Vipi! Kwa nini hakuna aliyenifahamisha kuhusu suala hili? Mbona ni mara ya kwanza kujifunza kuhusu swala hili?'," alisema Acaroglu.

"Siwezi kueleza jinsi nilivyohisi," alisema. Kwa hivyo, Acaroglu aliamua maishani  mwake analenga kubuni michoro endelevu na kuwasaidia watu kutengeneza bidhaa bora na kutoa huduma zitakazokuwa na madhara machache kwa mazingira.

Leo hii, Acaroglu ni mshindi wa Tuzo la Bingwa wa Dunia linalotolewa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa kutokana na juhudi zake za kueneza michoro yenye suhuhu endelevu. Ana imani ya dhati kuwa tuko katikati ya kipindi cha mabadiliko ya kitamaduni kuelekea uchumi unategemea nishati jadidifu kutokana na ukosefu wa mbinu mbadala za kutumia katika sayari yetu.

“Kuna changamoto ya kiubunifu itakayotuwezesha kubadilisha jinsi tunavyofanya mambo. Kubuni michoro siyo tu kubuni kiti kizuri sana, kubuni michoro ni kuchukua rasilimali yoyote na kuunda kitu kipya," alisema. "Tunajiandaa kutofaulu iwapo hatutajitokeza na mfumo unaotegemea nishati jadidifu.” 

image

Acaroglu, mwenye umri wa miaka 36 na mwanzilishi wa vituo viwili vya kubuni michoro—mojawapo kinashughulikia hali zinawezesha kampuni kupokea mafunzo ya kuziwezesha kutumia nishati jadidifu—anasema kuwa mifumo mingi ya biashara inayorurusiwa na serikali kubuniwa ni "isiyoweza kubadilika."

"Hatuna sera zinazounga mkono aina ya ubunifu unaotumia njia anuai katika jamii. Ni nchi chache tu ulimwenguni zinazoruhusu hili kutokea," alisema.

Falsafa yake ni kuwa badala ya kuuza tu bidhaa, ambavyo ni kazi ya mtumiaji kuvitupa akimaliza kutumia, kampuni ni sharti ziunde bidhaa vya misimu yote, vinavyoweza kutumiwa tena na vyenye manufaa ya kiuchumi kutokana na uwezo wa kutumika tena, tangu mwanzo.

Acaroglu anasema njia mwafaka ya kuchunguza madhara ya bidhaa kwa mazingira ni kutathmini mda wa matumizi yake kabla ya kuharibika, kwa sababu inaangalia athari ya vitu vinayoathiri uchumi tangu kutengenezwa hadi kutumika kwake.

Mbali na kutoa mafunzo kwa kampuni, pia ameunda thecircularclassroom.com kuwasaidia wanafunzi kufikiri tangu wakiwa na umri mdogo kuhusa bidhaa zinazoweza kutumiwa tena na wala si za matumizi ya mara moja. Aliundia nchi ya Ufini mtaala na sasa hivi anaundia nchi ya Thailandi mfumo mzima wa kufunzia, utakaotumika kando na ule utumikao shuleni.

"Mfumo wetu mbaya wa elimu haujengei vijana uwezo wa yale wanaohitaji kubuni uchumi mpya tunaouelekea," alisema.

Anasema yeye ni ashiki mkubwa wa Buckminster Fuller—wa maono ya siku za usoni aliyekuwa maarufu miaka ya 1950 kwa kubuni 'geodesic dome'—Acaroglu alisema kulichomvutia zaidi na Fuller ni uwezo aliokuwa nao wa kuathiri watu kuhusu mambo ya siku zijazo na jinsi ya kuleta mabadiliko ulimwenguni.

"Tunaishi kwa hali isiyoeleweka," alisema. "Hakuna chochote kinachoweza kutupa motisha katika hii dunia. Tunao uwezo wa kuharibu au kubuni katika hali hii."

Mabingwa wa Dunia, tuko kuu linalotolewa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, huwatambua watu mashuhuri kutoka kwa sekta na umma na za kibinafsi, na kutoka kwa mashirika ya uraia ambao kazi zao zimeleta mabadiliko chanya kwa mazingira. Iwapo unamfahamu mtu wa aina hii, mchague ili awe Bingwa wetu anayefuata.