23 Mar 2020 Tukio Ocean & Coasts

Shughuli tano za kuvutia unazoweza kutumia kufunza watoto wako kuhusu uchafuzi wa plastiki

 

Kwenda shuleni na mikutano vimesitishwa kote duniani kutokana na mkurupuko wa virusi vya korona (Covid-19) . Wakati mwingine, inaweza kuwa vigumu kushirikisha watoto wako katika shughuli ambazo zitawavutia kwa mda mrefu hasa ikiwa wewe pia unafanya kazi kutoka nyumbani. Hapa kuna baadhi ya mawazo ya kile unachoweza kufanya na watoto wako nyumbani ili kuwafundisha kuhusu tatizo la uchafuzi wa plastiki.  

Wazo la kwanza: tengeneza ala za muziki kutoka kwa uchafu wa plastiki

Kila mwaka tani milioni 8 za uchafu wa plastiki hutupwa baharini. Katika mwaka wa 2018, Shady Rabab kutoka Misri alishinda tuzo kuu la Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) Tuzo la Vijana Bingwa Duniani kwa kuchukua fursa ya kuondoa watoto mitaani na kukomesha matumizi mabaya ya plastiki. Alianzisha Garbage Conservatoire, iliyomwezesha yeye na watoto katika bendi yake kusafiri katika maeneo mbalimbali na ala zao za mziki zilizotengenezwa kutoka kwa uchafu wa plastiki. Hii ilionyesha dunia kuwa taka si uchafu hadi bali itakapotumiwa vibaya.

Himiza watoto wako kutumia taka (safi) ya plastiki kuunda ala zao za muziki. Wanaweza hata kukuandalia tamasha au kuweka kwa mitandao ya jamii. Bonyeza hapa ili kuona baadhi ya ala unazoweza kutengeneza

Shady Rabab with a flute made from an old plastic bottle. Photo by UNEP
Shady Rabab na filimbi yake iliyotengenezwa kutoka kwa chupa ya plastiki. Picha na UNEP

Wazo la pili: angalia kwenye kabati yako na upange vyombo kwa kuzingatia bidhaa zilizotumika kuvitengeneza.

Kila siku, tunatumia bidhaa nyingi za plastiki bila kujali madhara yake kwa mazingira. Wewe na watoto wako enda kabatini mwako halafu uwaelekeze kupanga vyombo vyote kwa kuzingatia bidhaa zilizotumika kuvitengeneza (plastiki, kadibodi, alumini na kadhalika.) Ambia watoto wako watenge vitu vianyoweza kutumiwa tena na tena na uwaonyeshe waangalie iwapo vina maandishi yanayoonyesha iwapo vinaweza kutumiwa tena au la.  Programu ya Usafishaji wa Bahari ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa  inaweza kutoa maelezo zaidi kwa watoto kuhusu aina mbalimbali ya plastiki na jinsi wanavyoweza kuzitumia.

Wazo la tatu: tenga siku ya kukabiliana na plastiki

Kuna uwezekano wa kutotoka nyumbani lakini haimaanishi kuwa huwezi kufanya hivyo ukiwa nyumbani. Kuanzia kwa vitu vya kupangusia watoto hadi kwa brashi za kusugulia zilizo na chembechembe za plastiki (vipande vidogovidogo vya plastiki vilivyo na milimita chini ya tano). Plastiki imejificha ndani ya vitu vingi tunavyotumia nyumbani. Hapa unaweza kuona baadhi ya vitu vinavyosababisha uchafu wa plastiki katika bafu lako. Njia mwafaka ya kukabiliana na plastiki iliyojificha ni kutenga siku kama familia ya kukabiliana na plastiki. Unaweza kufundisha watoto wako jinsi ya kujitengenezea brashi za kusafishia kutoka kwa mafuta ya nazi na kutoka kwa sukari na chumvi. Pia unaweza kuunda vitu vya kurembesha uso kwa kutumia asali na ndizi. Jiandalie mapochopocho, achilia muziki mzuri, kisha tulia.

Pixabay
Vitu vya kujitengenezea vya kurembesha uso, Picha na Seksak Kerdkanno, Pixabay

Wazo la nne: unda boti kutoka kwa taka ya plastiki.

Vitu vingi ambavyo viko karibu kutupwa vinaweza kuundwa na kutumiwa tena. Kutumia plastiki uliyokuwa umepanga kutupa kwa kusaidia mtoto wako kutengeneza chelezo au boti. Wanaweza kuweka vitu hivi kwa hodhi au kwenye sinki kuona iwapo vitaelea na hata kuweka vitu vyao kwenye boti inapoelea! Ikiwezekana wapeleke kwenye bwawa lako au mto ulio karibu ili washindane.

Kampeni ya hivi majuzi ya kusafisha bahari (Clean Seas campaign) walishindana kwa kutumia chelezo walizotengeneza. Dau la upana wa mita tisa lililotengenezwa kutoka kwa tani 10 za taka zilizokusanywa ufuoni mwa bahari nchini Kenya linalojulikana kama “Flipflopi” liliendeshwa kutoka Lamu nchini Kenya hadi Zanzibar huku uhamasishaji ukitolewa kuhusu uchafuzi wa plastiki.

Pixabay
Uchafu wa Plastiki, Picha na Stux, Pixabay

Wazo la tano: andaa shindano la mtindo wa nguo zilizotengenezwa kutoka kwa takataka

Kurekebisha—au “kuunda fanicha mpyabidhaa zingine, na kadhalika kutoka kwa kutumia vifaa kuukuu au vilivyotumika au kutoka kwa taka”—ni mtindo mzuri unaojali mazingira. Katika mwaka wa 2016, mmarekani Rob Greenfield alivalia nguo zote alizotengeneza kutoka kwa taka kwa kipindi cha mwezi mzima. Alishona suti za kupendeza. Kwa nini usiwaruhusu watoto wako wabuni mtindo mzuri wa mavazi kutoka kwa uchafu wa plastiki. Wanaweza kukuandalia tamasha la mtindo wa mavazi kutokana na ubunifu wao!

Kuna njia nyingine zaidi unazoweza kutumia kufundisha watoto kuhusu uchafuzi wa plastiki na madhara yake. Tovuti ya UNEP ya Clean Seas website inatoa ushauri wa kupunguza matumizi ya plastiki, na kuonyesha madhara yanasababishwa na uchafuzi wa plastiki.

Mkuu wa Uhamasishaji wa UNEP, Atif Butt anasema, "Sasa, kuliko kipindi kingine chochote, ni wazi kuwa ni sharti tushirikiane kufanya kazi ili tuweze kutatua changamoto kuu zinazoikabili dunia. Kwa kufundisha kizazi kijacho na kujifunza kutoka kwa vijana kuhusu changamoto za mazingira, tunaweza kupiga hatua kubwa katika juhudi za kukomesha uchafuzi."

Kampeni ya Clean Seas

Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa lilizindua Kampeni ya Clean Seas katika mwaka wa 2017 na lengo la kuleta pamoja vuguvugu la kimataifa litakalobadilisha jinsi plastiki inavyotumika kwa kupunguza plastiki inayotumiwa tu mara moja na kukabiliana na chembembechembe za plastiki zinazoongezwa kwa bidhaa bila kukusudiwa. Tangu wakati huo, nchi 60 zimeahidi kufanya juhudi za kuboresha ushughulikiaji wa plastiki kupitia kupunguza matumizi ya plastiki inayotumika tu mara moja. Jifahamishe zaidi kuhusu kampeni hiyo na jinsi unavyoweza kusaidia, amua kushirikiana na wabia wa kimataifa kukabiliana na uchafuzi wa bahari na ufuatilie kampeni zetu katika mtandao wa kijamii @UNEP kupitia InstagramFacebookTwitter na LinkedIn.