18 Nov 2019 Tukio Haki na usimamizi wa mazingira

Wanafunzi kutoka Kenya wafundishwa kuhusu sheria kuhusiana na mazingira

Katika dunia iliyo na utandawazi, changamoto za mazingira zinahitaji kushughulikiwa kwa njia mwafaka zinazodumisha amani, haki, maendeleo na inayowezesha utekelezaji wa haki za mazingira na haki za binadamu. Ni wajibu wetu sisi sote; na sote tuna haki za kuzishughulikia. Sisi wote ni  viongozi ambao sayari inahitaji.

Hayo ndiyo mambo kikundi cha vijana kutoka Kenya waliambiwa katika mwezi wa Oktoba mwaka wa 2019 wakati waliposhiriki katika mhadhara kuhusu sheria inayohusiana na masuala ya mazingira katika Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP).

UNEP huimiza kuwepo na uwajibikaji wakati wa kutunza mazingira kwa kuwawezesha wanaothiri utunzaji wa sheria, utunzaji wa sera na taasisi zinazoweka kanuni ya jinsi watu wanavyopaswa kuishi kwa kujali mazingira.

Wataalamu wa UNEP walifundisha wanafunzi kuhusu uongozi na utekelezaji wa sheria za kimataifa kuhusiana na mazingira kwa jumla. Sheria za kimataifa kuhusiana na mazingira zinaweza kushirikisha nchi nyingi kam ilivyo katika Mkataba wa Paris, au nchi chache kama ilivyo katika mikataba ya kimaeneo. Vyanzo vya sheria za kimataifa kuhusiana na mazingira vinaweza kuwa na malengo tofautitofauti kama vile ilivyo na Mkataba wa Ubayoanuai wa Viumbe Hai, au uwe dhahiri  kuhusiana na masuala fulani kama ilivyo na Makubaliano kuhusu Kuhifadhi kwa ndege aina ya Albatros na Petrel. Tunahitaji sheria za kimataifa kuhusiana na mazingira kwa sababu changamoto nyingi za mazingira huvuka mipaka ya taifa, ni ya kikanda na ya kimataifa. Masuluhisho yanahitaji ushirikiano wa kimataifa na utumiaji wa sheria zilezile kwa kila mtu.

Wanafunzi na wataalamu wa UNEP walizungumia kuhusu udhaifu na manufaa ya sheria za kimataifa kuhusiana na mazingira na wakajadili jinsi ambavyo wanafunzi wanaweza kushiriki zaidi katika utatuzi wa changamoto za mazingira. Wanafunzi walisema kuwa mhadhara huo ulikuwa na manufaa mengi na wakasema wamepewa changamoto ya kufikiria kuhusu vipengele vipya na tofautitofauti vya sheria za kimataifa kuhusiana na mazingira.

Baadhi ya mada zilizojadiliwa ni pamoja majukumu mbalimbali ya makundi tofautitofauti kuhusiana na usimamiaji na bayoteknolojia ya mazingira, kanuni ya kuwa ya majukumu mbalimbali yanayolenga kutekeleza wajibu uleule, na uchafu wa plastiki na mafunzo yanayotakana na upikaji marufuku wa plastiki nchini Kenya.

Kuhakikisha kuwa wanaendelea kuelimishwa licha ya mhadhara kuhitimika, UNEP ilishiriki na wanafunzi rasimali za kusoma.

James Nyaro, mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, alisema kwa niaba ya chuo: "Mlituruhusu kuwauliza masuali...nanyi mkayajibu kwa mapana na marefu...na hatuwezi kuchoka kuwashukuru.”

image

Ninapaswa kufahamu nini kuhusu sheria za kimataifa kuhusiana na mazingira

Mataifa yanaposhirikiana kuunda na kutekeleza sheria za kimataifa kuhusiana na mazingira, yanaweza kufanya mambo makuu. Tambiko la ozoni linaendelea vizuri kuimarika kabisa kipindi hiki na hii itaokoa watu milioni mbili kutopata saratani kila mwaka kufikia mwaka wa 2030. Mafanikio haya yanatorajiwa kupatikana kutokana na sheria za kimataifa kuhusiana na mazingira kupitia Mkataba wa Montreal unaohusiana na mazingira.

Kwa kuwa kila mtu ana haki ya kushiriki katika utunzaji wa mazingira, ni sharti sisi sote tuwe na uelewa wa sheria husika. Ijapokuwa ni wajibu wa kila taifa kuamua na kutekeleza sheria za kimataifa kuhusiana na mazingira, mwananchi wa kawaida anaweza kusahaulika wakati wa kuziunda na kuzitekeleza. Kama wananchi, ni sharti tuathiri maendelezi na utekelezaji wa sheria za kimataifa kuhusiana na mazingira, ili kuhakikisha zinakabiliana kwa njia mwafaka na changamoto tunazokumbana nazo. UNEP inahimiza kila mtu kujielimisha kuhusu sheria za kimataifa kuhusiana na mazingira na jinsi zinavyoathiri nchi zao kupitia,  InforMEA. Elimu ni hatua ya kwanza ya utekelezaji wa sheria za kimataifa kuhusiana na mazingira zinazotuhusu.

Tarehe 23 Oktoba mwaka wa 2019, wanafunzi wa maosomea shahada ya pili na ya tatu kutoka kitivo cha Usalama, Diplomasia na Elimu kuhusu Amani kutoka katika Chuo Kikuu cha Kenyatta walifundishwa kuhusu sheria za kimataifa kuhusiana na mazingira na wataalamu wa UNEP.

Maudhui Yanayokaribiana