Kazi yetu katika eneo la Asia Magharibi

Dhima ya afisi ya eneo la Asia Magharibi ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa ni kutoa uongozi na kutafuta wabia wa kutunza mazingira kupitia kushauri, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu katika eneo la Asia Magharibi kuboresha maisha yao bila kuathiri yale ya vizazi vijavyo.

Kazi yetu kuu ni kusimamia miradi ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa katika eneo hili.  Hii inamaanisha kuwa tunafanya kazi kwa kuleta pamoja nchi katika eneo hili na vitengo na vituo mbalimbali vya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa. Pia, tunahimiza kuwepo kwa ushirikiano na ubia na mashirika yanayojihusisha na maendeleo endelevu katika eneo la Asia Magharibi.

Afisi ya kanda inapatikana Bahrain na ina wataalamu wanaotoa ushauri kuhusu mazingira na ushauri wa kuifundi, wanahakiki mapendekezo, na kushauri kuhusu hatua zinazoweza kuchukuliwa na serikali na mashirika mengine.