Katika mwaka wa 2022, UNEP ilijiunga na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuimarisha juhudi za kukabiliana na changamoto za aina tatu duniani kwa kushughulikia afya ya binadamu, wanyama, mimea na mazingira kama changamoto moja iliyounganishwa. Muungano wa mashirika manne ya UNEP, FAO, Shirika la Afya Duniani (WHO) na Shirika la Afya ya Wanyama Duniani (WOAH) ulitoa Mpango wa Utekelezaji wa Pamoja wa Afya Jumuishi - mpango wa miaka tano ambao unalenga kuimarisha mifumo ya afya na kukabiliana na janga la magojwa yanayoambukizwa kutoka kwa wanyama, magonjwa yaliyopuuzwa ya kitropiki na yanayoenezwa na vekta, hatari za usalama wa chakula na vimelea sugu.
