Ripoti ya Hali ya Fedha za Kufadhili Mazingira Mwaka wa 2022 ya UNEP ilibainisha kuwa serikali, mashirika ya biashara na taasisi za fedha zinahitaji kuongeza uwekezaji wao wa kila mwaka mara tatu zaidi ili kudhibiti ongezeko la joto duniani, kukomesha kupunguza uharibifu wa bayoanuai, kukomeha uharibifu wa ardhi na kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu. Mtiririko wa fedha za kutoa suluhisho kutokana na mazingira kwa sasa ni dola za Marekani bilioni 154 kwa mwaka - theluthi moja ya dola bilioni 484 zinazohitajika kila mwaka kufikia mwaka wa 2030.
UNEP inashirikiana na wabia kufadhili miradi ya mazingira. Kwa mfano, Kituo cha Bidhaa Zinazowajibikiwa kinachoungwa mkono na UNEP kilikusanya zaidi ya dola za Marekani milioni 11 kupitia uwekezaji kutoka kwa maduka makubwa nchini Uingereza na Ireland Kaskazini ili kuwatia moyo wakulima wa Brazili kutokata miti- wakati wa kilimo cha soya. Wakati uo huo, Mpango wa Kukuza Viwanda vya Kuboresha Mifumo ya Ekolojia wa UNEP, unaosaidia mashirika madogo ya biashara ndogo na ya kati kushiriki uboreshaji wa mifumo ya ekolojia, ulikaribisha kundi jipya lililo na makazi yake nchini Kenya na kupanua shughuli zake hadi nchini Viet Nam kwa kuzindua Programu Endelevu ya Kukuza Biashara ya Misitu.
