UNEP ilisaidia Amerika ya Kusini na Karibia develop kuunda Mpango wa Utekelezaji wa Kanda kuhusu Ubora wa Hewa kuanzia 2022 hadi 2025. Katika kikao cha 18 cha Kongamano la Mawaziri wa Mazingira wa Afrika unaosimamiwa na UNEP, nchi 54 za Afrika ziliahidi kutokomeza utupaji na uchomaji wazi wa taka. Katika Asia ya Pasifiki, Kamati ya Mazingira na Maendeleo ya Tume ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi na Jamii ya Asia na Pasifiki ilipitisha tamko la mawaziri kuhusu kutekeleza Mpango wa Kikanda wa Kushughulikia Uchafuzi wa Hewa, UNEP akiwa mshauri.
Mwezi wa Januari, Kambodia ilizindua Mpango wake wa kwanza wa Hewa Safi. Mpango huu unalenga kupunguza kwa asilimia 60 za uzalishaji wa PM2.5 na uzalishaji gesi nyeusi ya ukaa, asilimia 24 ya uzalishaji wa methani na asilimia 18 ya uzalishaji wa kaboni dioksidi kufikia mwaka wa 2030. Inaweza pia kusaidia kuzuia hadi vifo 900 vya mapema kwa mwaka. Kwa usaidizi kutoka kwa CCAC, Kambodia imeanza kutekeleza viwango vya yuro 4/IV vya uzalishaji wa gesi chafu wa magari na ubora wa mafuta.
UNEP pia imeunga mkono Mataifa ya Afrika Magharibi na Afrika Mashariki kuweka viwango vya magari ambavyo vitapunguza uagizaji wa magari makuukuu, yanayochafua mazingira. Jumuiya ya Kiuchumi ya Wanachama 15 wa Nchi za Afrika Magharibi imepitisha kanuni zinazofanya uagizaji wa magari uzingatie viwango vya EURO 4/IV. Katika mwaka wa 2022, UNEP ilianza kusaidia nchi kufanyia kazi ahadi hizi na kuzifanya viwango vya kitaifa. Nchi tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki zilipitisha viwango sawia. Na ushauri kutoka kwa UNEP, Umoja wa Ulaya pia umeanza kurekebisha maagizo yake kuhusu magari yalioachwa kutumika.
Kwa ushirikiano na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na Taasisi ya Hali ya Hewa ya Ufini, UNEP ilifanya utafiti wa kwanza kabisa kuhusu vyanzo vya uchafuzi wa hewa katika mji mkuu wa Kyrgyzstan, Bishkek. Utafiti huo ulibainisha uchafuzi wa hewa kutoka majumbani kutokana na kupika kwa kutumia makaa ya mawe yalio na salfa kama chanzo kikuu ya uchafuzi wa hewa, kiwango zaidi kuliko uchukuzi au kituo cha umeme jijini, mambo ambapo hapo awali yalizingatiwa kuwa vyanzo vikuu. Matokeo hayo yaliunga mkono maamuzi ya benki za maendeleo ya kuelekeza uwekezaji kwa upunguzaji wa uzalishaji wa gesi chafu kutoka kwa sekta muhimu, kama vile kupasha joto kwenye eneo la makazi.
