Katika maadhimisho ya 35 Itifaki ya Montreal kuhusu Vitu Vinavyoharibu Tabaka la Ozoni yaliyoandaliwa na UNEP, utafiti ulionyesha kuwa makubaliano haya yalizalisha manufaa mengi kwa mazingira kuliko ilivyotarajiwa. Utafiti mmoja unaonyesha kuwa Itifaki hii inaweza kuwa ilizuia ongezeko la joto la 1.7 kufikia mwishoni mwa karne kwa kupiga marufuku vitu vinavyoharibu ozoni vinavyochangia ongezeko la joto duniani.
Utafiti huo ulibaini kuwa, bila Itifaki ya Montreal, mionzi ya urijuani ingeweza kuharibu mifumo ya ekolojia, na kusababisha kutolewa kwa tani bilioni 690 za gesi ya ukaa ambayo kwa sasa inahifadhiwa katika mimea na udongo. Ongezeko la ziada la joto lililoepukwa lilikadiriwa kuwa kati ya nyuzijoto 0.5 na nyuzijoto 1. Chini ya Marekebisho yake yaliyofanyika Kigali, Itifaki inazalisha matunda zaidi kwa kupunguza hidrofluorocarbons, gesi ya ukaa yenye nguvu, na kuongeza matumizi mazuri ya nishati ya vifaa vya kupunguza joto.
