Katika mwezi wa Juni, Kongamano la Stockholm+50 liliadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa vuguvugu la mazingira katika Kongamano la Stockholm la Mwaka wa 1972. Pia lilileta ulimwengu pamoja ili kuimarisha juhudi kuhusiana na Malengo ya Maendeleo Endelevu. Ajenda ya Utekelezaji, Uuishaji na Imani ya hafla hiyo iliweka wazi hatua 10 za kuchukuliwa ili kufikia sayari bora. Siku chache baadaye, Siku ya Mazingira Duniani

ilishirikisha zaidi ya watu milioni 65 na kushuhudia ahadi nyingi kutoka kwa serikali na sekta binafsi, ikiwa ni pamoja na Sweden kupiga marufuku leseni mpya za uchimbaji wa makaa ya mawe, mafuta na gesi asilia.

Tags
Image
Picha: Getty Images
Number of columns
One
image credit color
white