Kupitia Muungano wa Benki wa Net-Zero ulioitishwa na UNEP, zaidi ya benki 60 ziliweka malengo ya kisayansi ili kuondoa gesi ya ukaa kwenye orodha ya fedha zinazowekwa kwa faida, ikiwa ni pamoja na uwekezaji katika sekta ya makaa ya mawe na gesi. Zaidi ya nusu ya muungano huo umeweka malengo ya muda ya kuondoa gesi ya ukaa kufikia mwaka wa 2030 yanayoendana na lengo la nyuzijoto 1.5 la Mkataba wa Paris. Katika miezi 18 ya kwanza, muungano huo, unaosimamiwa na Mpango wa Fedha wa UNEP (UNEP FI), umekua na kufikia zaidi ya benki 120, zikiwakilisha karibu asilimia 40 ya mali inayomilikiwa na benki duniani.

Chombo Kinachotoa Mtaji, mfuko wa ubia anuai unaosimamiwa na UNEP, katika mwezi wa Julai ulishuhudia ujenzi ukianza katika mradi muhimu ulioufadhili: kiwanda cha kuzalisha umeme kutumia maji nchini Zimbabwe. Uzinduzi wa mtambo wa 5 MW unatazamiwa kufanyika mwaka wa 2023. Kwa ujumla, SCAF II, awamu ya pili ya kituo hicho, imesaidia miradi katika nchi 14 kote barani Asia na barani Afrika. Miradi hii inatarajiwa kupunguza karibu tani milioni 4 za kaboni dioksidi kwa mwaka na kubuni nafasi za kazi takribani 14,000.

Tags
Image
Fedha za miradi kama vile mitambo inayotumia umeme wa maji ni nguzo muhimu ya Chombo Kinachotoa Mtaji kinachosimamiwa na UNEP. Picha: iStockphoto
Number of columns
One
image credit color
white