Huku nchi zinazoendelea zikitarajiwa kuongeza magari bilioni 1 kufikia mwaka wa 2050, juhudi zinahitajika ili kuhakikisha magari hayo mengi yanazalisha kiwango cha chini au kutozalisha gesi chafu. Katika mwaka wa 2022, UNEP ilizindua Programu yake ya Usafiri wa Kutumia Umeme Dunianial, inayosaidia nchi 50 za kipato cha chini na cha kati kuacha kutumia mafuta yanayotokana na visukuku na kuanza kutumia magari ya umeme.

Kwa mfano, Ushelisheli inatekeleza mradi wa majaribio wa kutumia umeme kwa mabasi yake. Nchini Viet Nam, UNEP inasaidia huduma ya posta ya kuwasilisha bidhaa kuanza kutumia magari ya umeme ya magurudumu matatu. Na mpango huo unasaidia Chile kuhamishia mafanikio yake ya mabasi ya umeme mjini Santiago kwa miji mingine.

Tags
Image
Ukuaji wa sekta ya uchukuzi unahakikisha kuwa masuluhisho ya uzalishaji kidogo au kutozalisha kabisa yanahitajika ili kufikia malengo ya hali ya hewa. Picha: Getty Images
Number of columns
One
image credit color
white