Kuongezeka kwa matumizi mazuri ya nishati ni sehemu muhimu ya ajenda ya hali ya hewa, na mpango wa Kushirikiana Kutumia Vizuri (U4E) unaoongozwa na UNEP ulipiga hatua katika mwaka wa 2022. UNEP ilishirikiana na Pakistan kuweka kanuni zitakazopelekea kuokoa nishati ya 1.3 TWh kila mwaka kufikia mwaka wa 2030, pamoja na kupunguza uzalishaji wa hewa chafu kiwango sawa na kuondoa magari 630,000 ya abiria barabarani. Wakati uo huo, U4E ilisaidia Indonesia kuunda sheria ya mawaziri kuhusu kanuni zitakazowezesha kuokoa nishati kiwango sawa na kinachookolewa na Pakistan kila mwaka.

Juhudi hizi zinaendana na Mikakati ya Muungano wa Mataifa ya Kusini-Mashariki mwa Asia (ASEAN) ya Kuoanisha Viwango vya Bidhaa za Mwangaza, iliyotengenezwa na U4E. Kupitia utekelezaji wa viwango hivi, ASEAN inakadiriwa kuokoa 24 TWh ya matumizi ya umeme kila mwaka kufikia mwaka wa 2030. Hii inaweza kusaidia kupunguza tani milioni 18 za uzalishaji wa kaboni dioksidi kila mwaka na kuwezesha watumizi kuokoa zaidi ya Dola za Marekani bilioni 2 kwa matumizi ya umeme kila mwaka.

Tathmini ya Akiba ya Nchi ya U4E ya Mwaka wa 2022 inaonyesha kuwa ikiwa nchi zote zinazoendelea na zilizo na chumi zinazokua zitapitisha viwango vya chini vya nishati kwa kutoa mwanga, zaidi ya TWh 122 za matumizi ya umeme zitaokolewa kila mwaka kufikia mwaka wa2030, kiwango sawa na nishati inayozalishwa na vituo 55 vya umeme.

Tags
Image
Wateja nchini Chile wanaweza kufanya biashara ya friji zisizotumia nishati nyingi zilizoundwa kwa njia endelevu zaidi chini ya mpango wa U4E. Picha: Fundación Chile
Number of columns
Two
image credit color
white