
Ujumbe kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP
Kupitia njia nyingi, 2022 ulikuwa mwaka wa juhudi mpya za kushughulikia mazingira. Kuelekea mwanzoni mwa mwaka, katika Kikao cha Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa, Nchi Wanachama zilipitisha maazimio ya kihistoria ya kuimarisha juhudi za kukabiliana na uchafuzi, kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na kutunza na kuboresha mazingira kote ulimwenguni. Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi wa mwaka wa 2022 ulichangia historia kupitia kuanzishwa kwa mfuko wa hasara na uharibifu. Majadiliano ya kimataifa ya kukomesha uchafuzi wa plastiki yalianza nchini Uruguay. Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilitambua haki ya watu wote kuwa na mazingira safi, bora na endelevu. Na mwaka ulipoisha, Kongamano la Umoja wa Mataifa la Bayoanuai mjini Montreal lilipelekea kupitishwa kwa mfumo kabambe wa kutunza na kuboresha bayoanuai kufikia mwaka wa 2030. Mwaka huu pia ulishuhudua maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na kongamano la Stockholm+50.
Hata hivyo ulikuwa pia mwaka wa changamoto nyingi. Madhara makubwa ya changamoto za aina tatu duniani za mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa mazingira na bayoanuai, na uchafuzi na taka vilichangiwa na kuongezeka kutokana na ukosefu wa usawa, vita nchini Ukraine na kupanda kwa bei ya chakula na ya nishati. Kama kawaida, maskini na walio hatarini zaidi waliathiriwa zaidi na ukame, mafuriko, mioto misituni, kupungua kwa bayoanuai na kuongezeka kwa viwango vya uchafuzi.
Kama ripoti hii inavyoonyesha, shirika lilianza kutekeleza mkakati wake mpya, mkatati wa 2022-2025. Lilipata ushindi kwa kukabiliana na changamoto za aina tatu kwa sayari na kusaidia dunia kuanza kutekeleza ahadi zake za kuboresha mifumo ya ekolojia, kupunguza shinikizo la uchafuzi wa hewa na kulinda mamilioni ya watu katika mataifa yanayoendelea walio hatarini kuathiriwa na hali ya hewa.
Basi, haishangazi kwamba mahitaji ya kuchukuliwa kwa hatua badala ya kutoa ahadi tu yanazidi kuongezeka. UNEP iliimarisha juhudi za kukabiliana na majanga haya na kuanza kutekeleza mkakati wake, mkakati wa 2022-2025. Kwa kuzingatia uwezo wa wabia wake, UNEP ilifanya kazi na Nchi Wanachama kutimiza ahadi za kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kutunza na kuboresha mifumo ya ekolojia, na kupunguza shinikizo la uchafuzi. Kupitia haya yote, UNEP inaendelea kuunga mkono nchi kutekeleza azimio la 4/17 la Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa kwa kujumuisha usawa wa kijinsia na haki za binadamu katika sera, mikakati, programu na miradi ya mazingira, hata inapoendelea kufanyia marekebisho mfumo wake wa kijinsia ili kutimiza kazi yake vyema.
Kama shirika, UNEP imejitolea kuwa shirika sikivu na linalojali. UNEP ilibadilisha mfumo wake wa kushirikiana na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa kupitia Vikosi vya Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa ili kushughulikia vyema vipaumbele vya Nchi Wanachama na Malengo ya Maendeleo Endelevu, na kuunda mifuko mipya tatu ya fedha inayotoa ufadhili unaoweza kubadilika ili kuwa na mazingira thabiti, kuishi kwa amani na mazingira na kutochafua sayari. UNEP pia ilifikia usawa wa kijinsia katika viwango vyote vya kitaaluma na ngazi za juu na kuboresha uanuai ya kijiografia wa wafanyikazi wake.
Lakini kazi kubwa iliyo mbele yetu ni kupunguza changamoto za aina tatu duniani. Kama mamlaka kuu ya kimataifa ya mazingira, UNEP itatoa shinikizo zaidi na kushirikiana kwa karibu zaidi na nchi, mfumo wa Umoja wa Mataifa, mashirika ya uraia na sekta binafsi ili kutoa masuluhisho na kufanya kazi ili kuwa na ulimwengu ambapo watu wote, popote walipo, wanaweza kufurahia haki yao kuwa na mazingira bora.
UNEP kupitia Takwimu
ni kiasi ambacho plastiki zinazoingia baharini zinaweza kupunguzwa kupitia hatua za uchumi unatumia bidhaa tena na tena, ikiwa ni pamoja na chini ya mpango wa kukabiliana na uchafuzi wa plastiki ulioanzwa kujadiliwa na mataifa mwaka wa 2022
idadi ya malengo madhubuti yanayohitaji kufikiwa kufikia mwaka wa 2030 chini ya mfumo mpya, Mfumo wa Bayoanuai Duniani
ni kiwango cha ongezeko zaidi la joto duniani ambalo linaweza kuepukika kupitia Mkataba wa Montreal kwa kutunza vitekaji vya gesi ya ukaa kutoka kwa mionzi ya urujuani
ni jumla ya idadi ya watu wanaotarajiwa kunufaika na kazi ya UNEP ya shushughulikia mifumo ya ekolojia kutegemea eneo
ni kiwango cha idadi ya magari yatakayoondolewa barabarani kila mwaka kupunguza uchafuzi wa hewa kupitia kazi ya mwanga bora inayoungwa mkono na UNEP nchini Pakistan na Indonesia
Ni kiwango cha taka iliyopatikana na kushughulikiwa mjini Mosul na kituo kipya cha kuchakata taka kinachoungwa mkono na UNEP
ni idadi ya watu walioshiriki katika Siku ya Mazingira Duniani
Kikao cha tano cha Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa
Wahusika wengi walikuwa na matokeo chanya zaidi katika awamu ya pili ya Kikao cha tano cha Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA 5.2) kilichofanyika mwezi wa Februari mjini Nairobi.
Tamko la kisiasa la UNEA 5.2 – hafla iliyohudhuriwa na zaidi ya watu 3,400 ana kwa ana na washiriki 1,500 mtandaoni - lilisisitiza umuhimu wa kusitisha kupungua kwa bayoanuai na kugawanyika kwa makazi. Maazimio juu ya asili yalishughulikia masuala kama vile bayoanuai na afya, usimamizi endelevu wa ziwa, na ufafanuzi wa jumla wa suluhu za asili. Maazimio kuhusu miundomsingi thabiti, kutochafua mazingira wakati wa kujikwamua na COVID-19 na masuala ya mazingira ya usimamizi wa madini na metali yaliimarisha umuhimu wa uchumi unatumia bidhaa tena na tena.
Hatua kubwa zilipigwa kuhusu kemikali, taka na uchafuzi. Azimio la kuanza kujadili kuhusu makubaliano ya kukomesha uchafuzi wa plastiki huziba pengo muhimu katika hatua za kushughulikia mazingira. Ijapokuwa azimio la kuanzisha jopo la sera ya kisayansi kuhusu usimamizi mzuri wa kemikali na taka, na kuzuia uchafuzi, litatoa kwa maswala haya muhimu chombo cha kisayansi sawia na vile vya hali ya hewa (Jopo la Serikali Mbalimbali kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi) na bayoanuai (Jopo la Sera ya Sayansi ya Serikali Mbalimbali kuhusu Bayoanuai na Huduma za Mifumo ya Ekolojia).
UNEA pia ilifanya kikao maalum cha Maadhimisho ya Miaka 50 ya UNEP
na kutathmini matunda ya ushirikiano wa kushughulikia mazingira katika kipindi cha miongo mitano iliyopita. Wakuu wa Nchi na wajumbe kutoka nchi 175 walitoa tamko la kihistoria na kuimarisha kujitolea kwao kushughulikia mazingira. Walitoa pongezi kwa kazi ya UNEP, ambayo imezaa matunda kama vile kutunza tabaka la ozoni na kukomesha matumizi ya petroli iliyo na risasi.
Sayari tayari ilikuwa inaonyesha dalili za kulemewa na mzigo wa binadamu tangu mwaka wa 1972 wakati shirika lilipoanzishwa. Katika miongo iliyofuata, UNEP na wabia wake walishirikiana na Nchi Wanachama kukabiliana na uchafuzi wa hewa, kurejesha tabaka la ozoni, kutunza bahari duniani, kukuza uchumi jumuishi usiochafua mazingira, na kutoa tahadhari kuhusu uharibifu wa bayoanuai na mabadiliko ya tabianchi. Kazi hiyo haijawahi kukosa kuwa na umuhimu zaidi.
Kushughulikia Sayari
Kushughulikia Mazingira
Kushughulikia mazingira
Azimio hilo litasaidia kupunguza uasi kwa mazingira, kuziba mapengo ya ultunzajii na kuwawezesha watu hasa walio katika mazingira hatari wakiwemo watetezi wa haki za mazingira, watoto, vijana, wanawake na watu wa kiasili.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres
UNEP ilitoa Tuzo kwa Sir David Attenborough Tuzo la Mabingwa wa Dunia katika kitengo cha Mafanikio ya Kudumu kutokana na kujitolea kwake kupitia utafiti, uhifadhi wa kumbukumbu na uhamasishaji kuhusu utunzaji na uboreshaji wa mazingira.
UNEP ilimtangaza nyota wa Aquaman na mwanaharakati wa masuala ya bahari Jason Momoa kama Mhamasishaji mpya wa Maisha Chini ya Maji katika Kongamano la Umoja wa Mataifa la Bahari.
Hatua za Kushughulikia Kemikali na Taka
Kupanua ufikiaji wa UNEP
Uwakilishi wa kijiografia na usawa wa kijinsia
UNEP imeunda mkakati wa kufikia rasilimali watu ili kuvutia vipaji vya vijana kutoka kwa Nchi Wanachama ambazo zina uwakilishi mdogo na vikundi vya kikanda visivyo na uwakilishi mkubwa. Kumekuwa na kuimarika kwa uanuai kikanda. Kategoria za kitaaluma na makundi yaliopo hapo juu yalishuhudia ongezeko la takriban asilimia 10 ya wafanyakazi kutoka Kundi la Asia ya Pasifiki na takriban asilimia 30 kutoka Kundi la Ulaya Mashariki. Katika mwaka wa 2022, UNEP ilifikia au kushinda kiwango kinacholengwa na Umoja wa Mataifa cha usawa wa kijinsia (asilimia kati ya 47 na 53) katika viwango vyote vya kitaaluma na zaidi.
Ufadhili mahususi
UNEP ilianzisha mifuko ya aina tatu ili kutoa ufadhili kutegemea hitaji ili kusaidia utekelezaji wa malengo ya Mkakati wa Muda (2022-2025) ya mazingira dhabiti, kuishi kwa amani na mazingira na kuwezesha kuw na sayari isiyo na uchafuzi. Dola za Marekani milioni 14 zilikusanywa kwa ufadhili wa aina hii katika mwaka wa 2022.
Ufadhili kutegemea hitaji utakamilishana na Mfuko wa Mazingira wa UNEP na kusaidia kuhama kutoka kwa ufadhili wa miradi mahususi hadi kwa ufadhili kutegemea hitaji ili kuimarisha athari. Michango kutoka kwa wabia kutika katika sekta binafsi na sekta ya umma itawezesha mbinu ya sayansi ya kina, hali itakayoaidia kusaidia kuimarisha kazi ya UNEP kama mamlaka ya kimataifa ya mazingira na kuwezesha shirika hili susaidia vyema Nchi Wanachama.
Ushirikishwaji wa sekta binafsi
UNEP imefanya uamuzi wa kimkakati wa kuwa na ushirikiano na sekta mbalimbali na sekta mtambuka na miradi katika sekta zilizo na athari kubwa. UNEP inashirikiana na mashirika ya sekta ya kibinafsi kupitia miradi zaidi ya 40 inayolenga nishati, plastiki, chakula na kilimo, huduma za afya, fedha na teknolojia ya habari. Sayansi ya UNEP inasaidia mashirika ya biashara kupata masuluhisho bora. Kwa mfano, Ubia wa UNEP wa Mafuta na Magari Yasiyochafua Mazingira – mradi kati ya sekta ya umma na binafsi iliyo na wabia 73 wanaokuza mafuta na magari yasiyochafua mazingira safi katika nchi zinazoendelea na nchi zilizo na uchumi unaokua – ulisaidia kukomesha matumizi ya petroli iliyo madini ya risasi.
Mfano mwingine ni Mpango wa Plastiki ya Utalii Duniani (GTPI) wa UNEP. Mpango huo una sahihi 121, na makadirio ya mapato ya kila mwaka ya zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 43. Katika mwaka wa 2021 na mwaka wa2022, GTPI ilikuwa na kampeni ya majaribio ya kuripoti kwa kampuni kubwa ambazo zilijiunga na mpango huo katika mwaka wa 2020 na ambayo ripoti ya kila mwaka ni sharti itolewe. Baadhi ya bidhaa za plastiki milioni 108 zimeacha kutumika katika mashirika yote ya biashara yanayoripoti.
Mabadiliko ya kidigitali
Muungano wa Uendelevu wa Mazingira wa Kidijitali (CODES) - muungano unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ulio na washikadau 1,000 - ulizinduliwa wakati wa Stockholm+50 ili kuunga mkono matumizi ya teknolojia ya kidijitali kushughulikia changamoto za iana tatu kwa sayari. CODES inalenga kuongeza idadi ya nchi na makampuni yanayoshirikiana kutekeleza mipango ya pamoja ya utekelezaji chini ya Mwongozo wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Ushirikiano wa Kidijitali.
UFADHILI
Hali ya Kifedha Mwaka wa 2022 kufikia tarehe 31 Desemba mwaka wa2022 (Mamilioni ya Dola za Marekani)
Bajeti
Mapato
Matumizi
- Bajeti ya kawaida ya UN
- Mfuko wa mazingira
- Fedha zilizotengwa
- Fedha za kimataifa
Michango Kuu 15 Iliyotengewa mwaka wa 2022 (mamilioni ya Dola za Marekani)
| Mfuko wa Mazingira Duniani | 321.5 |
| Ujerumani | 52.0 |
| Mashirika ya Umoja wa Mataifa | 34.6 |
| Uswidi | 30.3 |
| Mfuko wa Mashirika ya Kimataifa (Mkataba wa Montreal) | 22.6 |
| Marekani | 22.5 |
| Kamisheni ya Ulaya | 21.2 |
| Norwe | 21.1 |
| Mpango wa Fedha wa UNEP* | 18.5 |
| Wakfu / NGO | 15.0 |
| Uswisi | 11.8 |
| Uingereza | 9.9 |
| Mfuko wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi | 8.8 |
| Denmark | 8.7 |
| Kanada | 5.5 |
Wachangiaji 15 wakuu wa Mfuko wa Mazingira mwaka wa 2022 (mamilioni ya Dola za Marekani)
| Uholanzi | 8.4 |
| Ujerumani | 7.9 |
| Ufaransa | 7.6 |
| Marekani | 7.6 |
| Norwe | 7.0 |
| Denmark | 6.5 |
| Uswidi | 5.1 |
| Uingereza | 4.5 |
| Ubelgiji | 4.2 |
| Uswisi | 4.0 |
| Italia | 3.3 |
| Ufini | 2.7 |
| Canada | 2.5 |
| Japani | 1.5 |
| Uchina | 1.4 |
-
*
Ubia kati ya UNEP na sekta ya fedha duniani ili kutafuta ufadhili kutoka kwa sekta binafsi kwa maendeleo endelevu.
Wachangiaji wa Mfuko wa Mazingira (2022) kwa kategoria (idadi ya Nchi Wanachama)
- Waliochanga kikamilifu (44)
- Wachangiaji wengine (38)
- Wasiochanga (111)
Chapisho hili linaweza kunakiliwa lote au sehemu yake na kwa namna yoyote kwa madhumuni ya elimu au yasiyokuwa ya biasharaa bila ruhusa maalum kutoka kwa mmiliki wa hakimiliki imradi unaonyesha chanzo chake. Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa litafurahia kupokea nakala ya chapisho lolote linalotumia chapisho hili kama chanzo. Hairuhusiwi kuchapisha chapisho hili ili kuliuza tena au kwa madhumuni mengine yoyote ya kibiashara bila kibali kupitia maandishi kutoka kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa. Uteuzi wa mashirika kijiografia katika ripoti hii, na uwasilishaji wa makala humu, haimaanishi utoaji wa maoni ya aina yoyote kwa upande wa mchapishaji au mashirika yanayoshiriki kuhusu hadhi kisheria ya nchi yoyote, kanda au eneo, au ya mamlaka yake, au kuhusu uwekaji wa mipaka yake. Wa Kumtaja: Isipokuwa imeonyeshwa vinginevyo, data yote katika chapisho hili imetolewa kutoka kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa. Kwa taarifa zaidi: unep.org/annualreport.
© Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, 2023