Katika mwezi wa Desemba, katika Kongamano la Umoja wa Mataifa la Bayoanuai (mkutano wa 15 wa Kongamano la Nchi Wanachama wa Mkataba wa Uanuai wa Kibayolojia - COP15), Mataifa yalikubaliana juu ya mfumo mpya msingi wa kutunza bayoanuai - Mfumo wa Kimataifa wa Bayoanuai wa Kunming-Montreal, ukiwa na malengo manne na shabaha 23 za kupunguza uharibifu wa bayoanuai kufikia mwaka wa 2030. Shabaha - ambazo nyingi zinalenga kuimarisha haki za watu wa kiasili, ambao ni wasimamizi wakuu wa bayoanuai - ni pamoja na:

  • uhifadhi na usimamizi bora wa angalau asilimia 30 ya ardhi duniani, maji ya maeneo ya bara, maeneo ya pwani na bahari;
  • kukamilisha uboreshaji au kuhakikisha unaendelea kwa angalau asilimia 30 ya ardhi iliyoharibiwa, maji ya maeneo ya bara, na mifumo ya ekolojia ya maeneo ya pwani na baharini;
  • kupunguza kabisa uharibifu wa maeneo yenye umuhimu mkubwa kwa bayoanuai;
  • kuhakikisha manufaa kutokana na matumizi ya rasilimali za kijenetiki na taarifa za kidijitali kuhusu rasilimali za kijenetiki zinashirikiwa kwa haki na usawa;
  • kupunguza maradufu uharibifu wa chakula na kupunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya kupita kiasi ya bidhaa na uzalishaji wa taka;
  • kupunguza kwa nusu virutubishi vya ziada na hatari inayoletwa na viuatilifu na kemikali hatari;
  • kuondoa au kufanyia marekebisho ruzuku zinazodhuru bayoanuai kwa angalau dola bilioni 500 za Marekani kwa mwaka;
  • kukusanya angalau dola bilioni 200 za Marekani kwa mwaka katika ufadhili wa ndani ya nchi wa kimataifa; na
  • kuhakikisha kwamba makampuni na taasisi za fedha zinafuatilia, kutathmini na kufichua hatari zao, utegemezi na athari kwa bayoanuai.

Mfuko wa Ufadhili wa Mazingira Duniani utaanzisha hazina maalum ili kuimarisha ufadhili wa kutekeleza mfumo mpya. Hazina nyingine ya kimataifa itaanzishwa ili kusaidia ugawaji sawa wa manufaa ya taarifa za kidijitali kuhusu rasilimali za kijenetiki.

Mikataba mingine inayosimamiwa na UNEP kuhusu mazingra pia ilizalisha matunda katika mwaka huu. Kwa mfano, katika mwezi wa Novemba, Wanachama wa Mkataba wa Biashara ya Kimataifa ya Wanyamapori na Mimeapori Ilio Hatarini Kutoweka (CITES) walipitisha mapendekezo ya kudhibiti biashara ya kimataifa katika zaidi ya spishi 500 zaidi.

Tags
Image
Mradi wa kurejesha misitu nchini Kamerun, sehemu muhimu ya Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya ekolojia unaosimamiwa na UNEP. Picha: UNEP
Number of columns
Two
image credit color
white