Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia, unaosimamiwa na UNEP na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), unasaidia kutekeleza ahadi za kuboresha hekta bilioni 1 za ardhi, eneo lenye ukubwa sawa na China, kufikia mwaka wa 2030. Mwaka wa 2022, Muongo huo ulituza Miradi 10 za kwanza Anzilishi za Kuboresha Mifumo ya Ekolojia Duniani, zinazolanga kuboresha zaidi ya hekta milioni 68 - eneo kubwa kuliko Myanmar, Ufaransa au Somalia - na kubuni nafasi za kasi takribani milioni 15. Muongo utasaidia miradi hii kwa kuiangazia, kukuza mitandao, ufuatiliaji na ufadhili.
UNEP ilishirikisha umma katika uboreshaji kupitia Green Game Jam 2022, sehemu ya Muungano wa Kuchezea Sayari unaondeshwa na UNEP. Baadhi ya studio 38 za michezo zilifanyia marekebisho michezo yao ili kujumuisha mada za mazingira, na uwezekano wa kufikia karibu wachezaji milioni 276 wanaoshiriki kila mwezi. Kama matokeo ya juhudi hizi, karibu miti milioni 2.5 ilipandwa kupitia ushirikiano wa Ecosia na Ecologi.
Umoja wa Mataifa pia uliteua mwaka wa 2022 kuwa Mwaka wa Kimataifa wa Maendeleo Endelevu ya Milima ili kutoa tahadhari kuhusu uwezo wa mifumo ya ekolojia ya milima kuathirika. UNEP ilikuwa mwenyeji wa Mkataba wa Carpathian -mkataba unaolenga kutunza eneo la milima la Carpathian, Ulaya Mashariki - ulishinikiza kuchukuliwa kwa hatua kuhusu bayoanuai ya milima katika Kongamano la Umoja wa Mataifa la Bayoanuai.
