Mabingwa wa Dunia Mwaka wa 2023

Watu kote ulimwenguni wanajitokeza na mbinu bunifu za kukomesha uchafuzi wa plastiki na kuboresha sayari yetu. Mabingwa wa Dunia wako mstari mbele kwenye juhudi hizi. Wanatupa matumaini kuwa kuna masuluhisho kwa uchafuzi wa plastiki na kutukumbusha kuwa uendelevu wa mazingira ni muhimu katika kufikia maendeleo endelevu.