Constantino (Tino) Aucca Chutas, Bingwa wa Dunia Mwaka wa 2022 - Motisha na kuchukua hatua

Constantino (Tino) Aucca Chutas (Peru), ambaye pia ametuzwa katika kitengo cha Motisha na Kuchukua Hatua, ameanzisha mfumo wa upandaji miti katika jamii unaoendeshwa na wenyeji na jamii za kiasili. Hali ambayo imepelekea miti milioni tatu kupandwa nchini Peru. Pia anaongoza juhudi kabambe za upandaji miti katika nchi zingine za eneo la Andes.