Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa linafahamu umuhimu wa kushirikisha Makundi Makuu na Wadau wengine kama wabia na kujivunia mchango wao. Hutoa utafiti muhimu na uhamasishaji, na husaidia UNEP kufikia malengo yake mapana ya mda mrefu.

Maamuzi yanayotolewa na serikali mbalimbali yataungwa mkono na kutambuliwa mno na umma iwapo serikali zitazingatia maoni ya Makundi Makuu na Wadau mapema iwezekanavyo wakati wa michakato ya kubuni sera na kufanya uamuzi. Makundi Makuu na Wadau pia huchukua nafasi ya moja kwa moja wakati wa kuunda sera, kutoa mapendekezo, kufuatilia kwa makini au kuhamasisha.

Uhusiano kati ya UNEP na mashirika ya uraia umeimarika mno katika kipindi cha muongo mmoja uliopita. Kwa sasa zaidi ya NGOs 500 ni washauri rasmi. 

Mashirika ambayo yangependa kutumia fursa hii ili kuweza kusikika na UNEP yanaweza kushiriki moja kwa moja kwa kutuma ombi la Kuidhinishwa kwa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA). Hii itawezesha UNEA kuwa mwangalizi.

Kwa taarifa zaidi, tazama: