• Maelezo ya Jumla

Lini:  Novemba 18 - 24, 2022   

Wapi:  Kote duniani

Mashirika manne - Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO), Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Shirika la Afya Duniani (WHO), na Shirika la Afya ya Wanyama Duniani (WOAH, lililoanzishwa kama OIE)  wanafuraha kutangaza kaulimbiu ya Wiki ya Uhamasishaji kuhusu Antimikrobia Duniani (WAAW) Mwaka wa 2022:  'Kushirikiana kuzuia usugu dhidi ya antimikrobia'

Usugu dhidi ya antimikrobia (AMR) ni tishio kwa wanadamu, wanyama, mimea na mazingira.  Hutuathiri sisi sote.  Hii ndiyo sababu kaulimbiu ya mwaka huu inahitaji ushirikiano wa sekta zote ili kupelekea ufanisi wa dawa hizi muhimu.  Kukabiliana na AMR kunahitaji juhudi za kimataifa na lazima ishughulikiwe kupitia mbinu ya Afya Moja.

Kufanikisha haya, sekta zote zinapaswa kushirikiana na kuhimiza matumizi ya busara ya antimikrobia, pamoja na kuchukua hatua za kuzuia hali hii. Kuimarisha kinga na udhibiti wa maambukizi katika vituo vya kutolea huduma za afya, mashambani na kwenye viwanda vya chakula, kuhakikisha kuna upatikanaji wa chanjo, maji safi, usafi wa mazingira na usafi kwa jumla, kutekeleza matendo bora katika uzalishaji wa chakula na kilimo, na kuhakikisha kuna usimamizi mzuri wa taka na maji machafu kutoka sekta kuu ni muhimu katika kupunguza hitaji la dawa za kuzuia vimelea na kupunguza kuibuka na kusambaza AMR.   

Kaulimbiu ya Wiki ya Uhamasishaji kuhusu Antimikrobia Duniani inasalia kuwa 'Antimikrobia:  Tumia kwa Uangalifu'.  WAAW huadhimishwa kutoka tarehe 18 hadi tarehe 24 Novemba ya kila mwaka.

WAAW 2022