Sawfish, Photo by Petr Kratochvil

Kuhusu Mifumo ya Ekolojia

Binadamu hutegemea mifumo mizuri ya ekolojia kukidhi mahitaji yao muhimu, ila mahitaji muhimu ya watu wengi hayapatikani kwa njia endelevu.

Watu wapatao milioni 795 hukumbwa na baa la njaa na watu bilioni 1.2 huishi katika maeneo yasiyo na maji ya kutosha. Wakati uo huo, uharibifu wa bayoanuai unatarajiwa kuendelea, au hata kuongezeka. Kufikia mwaka wa 2030, dunia itahitaji asilimia 40 ya maji zaidi, asilimia 50 ya chakula zaidi, asilimia 40 ya nishati zaidi na asilimia 40 ya mbao na nyuzi zaidi. Njia tu ya pekee inayoweza kutuwezesha kukidhi mahitaji haya ni kupitia ushughulikiaji mzuri wa mifumo ya ekolojia kwa njia endelevu. 

Soma zaidi

Kazi yetu

Malengo ya Maendeleo Endelevu Yanayokaribiana

Watu na wabia

Kazi yetu inayohusiana na mifumo mizuri inayozalisha mazao inadhihirika kupitia miradi mbalimbali, ubia na vyombo vingine  muhimu. 

  • UNEP - Kituo cha Uhifadhi na Ufuatiliaji wake
  • UNEP - Ubia wa Kushughulikia Mifumo ya Ekolojia Duniani 
  • Tawi la Kushughulikia Mifumo ya Baharini na Maeneo ya Pwani 
  • Tawi la Kushughulikia Bayoanuai na Huduma kutoka kwa Mifumo ya Ekolojia
  • Tawi la Kushughulikia Maji Safi, Ardhi na Mabadiliko ya Tabianchi