Unsplash
15 Jul 2021 Hotuba Nature Action

Kuimarisha uchumi bila kuchafua mazingira ni muhimu barani Afrika

Unsplash

Kuimarisha uchumi bila kuchafua mazingira ni muhimu barani Afrika

Hotuba iliyoandaliwa kutolewa wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa Utekelezaji wa Hatua za Kuimarisha uchumi bila kuchafua mazingira na Tume ya Umoja wa Afrika

 

Mheshimiwa Felix Tshisekedi, Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Mheshimiwa Moussa Faki, Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika

Madamu Kamishna Joseph Sacko, Kamishna wa Uchumi wa Vijijini na Kilimo wa Tume ya Umoja wa Afrika

Waheshimiwa, Wakuu wa Nchi na Mawaziri wa Serikali.

Pokeeni salamu kutoka kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, lenye makao yake makuu ya pekee ya Umoja wa Mataifa yanayopatikana kwenye nchi zinazoendelea, mjini Nairobi, nchini Kenya. Nimetunukiwa fursa ya kuhutubia mkutano huu muhimu.  

Kwa kuwa na idadi kubwa ya vijana mahiri na wabunifu, Afrika ina uwezo wa kuwa na uchumi dhabiti duniani. Bara linashikilia asilimia 30 ya madini ambayo hayajatumiwa duniani. Asilimia 65 ya ardhi yake ni ya kilimo. Lina uwezo mkubwa wa kuzalisha nishati jadidifu. Lina rasilimali za uvuvi ambazo hazimilikiwi mno na watu binafsi. Kuanzia kwa bahari na maziwa hadi misitu ya mvua na ardhi ya mboji, bara hili linaloundwa na mataifa mengi na watu wengi lina uwezo mkubwa.

Lakini maono ya Afrika ya hatarini. Mdororo wa uchumi unaohusishwa na COVID-19 umegharimu zaidi ya nafasi za kazi milioni 30, umesababisha umasikini na madeni kuongezeka. Wakati uo huo, athari kwa mazingira - kutokana na hali mbaya ya hewa, uharibifu wa bayoanuai na uchafuzi wa mazingira - ni vitu vinavyorudisha bara nyuma.

Njia bora ya kushughulikia maswala haya kwa wakati mmoja ni kutoa kipaombele kwa uwekezaji usiochafua mazingira kama sehemu ya kujiimarisha baada ya COVID-19. Uwekezaji unaowezesha matumizi endelevu ya rasilimali. Unaowezesha matumizi ya nishati kwa njia bora isiyochafua mazingira na kotoa masuluhisho kutokana na mazingira. Unaowezesha kilimo kinachoendeshwa kwa njia endelevu. Unaobuni miji dhabiti ya kijani. Hii ndiyo sababu Mpango wa Utekelezaji wa Hatua za Kuimarisha uchumi bila kuchafua mazingira wa Muungano wa Afrika unakaribishwa.

UNEP iinaunga mno mkono Mpango wa Utekelezaji, ambao unaingiliana mno na Mpango wa Kushinikiza Kuimarisha uchumi bila kuchafua mazingira barani Afrika uliopitishwa na Mawaziri wa Mazingira barani Afrika kupitia AMCEN. Kupitia mfumo wa Uratibu wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa ulioboreshwa, UNEP iko tayari kufanya kazi na nchi barani Afrika kuleta mabadiliko yanayohitajika, ili kuunga mkono Malengo ya Maendeleo Endelevu na Ajenda 2063. Kupitia ufadhali wa serikali wa sera zisizochafua mazingira na matumizi ya fedha ndani ya taifa. Kupitia sheria zilizoimarishwa. Kupitia upatikanaji bora wa ufadhili endelevu na miundomsingi endelevu. Yote ni mambo muhimu wakati wa kuimarisha uchumi.

Kama chumi nyingine zote, uchumi wa Afrika umeathirika sana na janga. Kwa hivyo, tunapotoa wito wa mshikamano na haki kuhusiana na upatikanaji wa chanjo, ndivyo ni lazima tuombe ufadhili kupitia njia za jadi na njia za kisasa wakati huu muhimu. Kwa sababu idadi kubwa ya chumi ulimwenguni - ikijumuisha nchi za Kiafrika - zitatatizika kudumisha uthabiti wa chumi kuu. Ila tusijali, tuendelee kujiimarisha. Hata baada ya kuondolewa madeni, nchi zinazoendelea zinakabiliwa na shinikizo la kutumia malighafi, na kupuuzilia mbali matarajio ya kushughulikia uhifadhi na mabadiliko ya tabianchi. Na bila usawa wa upatikanaji wa chanjo, nchi nyingi zitashindwa kushughulikia masuala haya kutokana na COVID-19, na kushindwa kujiimarisha pasipo na kuchafua mazingira.

Kuimarisha uchumi bila kuchafua mazingira ni muhimu kwa kila taifa barani na kwa ulimwengu mzima. Kwa hivyo mshikamano wa kimataifa na kusaidiana ni muhimu ili kuwezesha kujiimarisha. Ni sharti tushirikiane kuhakikisha hatima ya afrika haibagui na wala hakuna kuchafua mazingira.

Asanteni.         

Inger Andersen

Mkurugenzi Mtendaji

 

 

covid-19 response logo