18 Jun 2019 Toleo la habari Nishati

Uwekezaji katika nishati jadidifu ulifikia dola za marekani bilioni 288.9, zaidi kuliko uwekezaji kwenye mafuta na gesi asilia

  • Uwekezaji duniani ulipungua kwa asili mia 11 ikilinganishwa na mwaka wa 2017, ikichangiwa kiasi na kuanguka kwa bei ya nishati ya jua.
  • Uwekezaji katika nishati jadidifu katika nchi nyingi zinazoendelea uliongezeka kwa asili mia 6 na kufikia dola za Marekani bilioni 61.6, kiwango cha juu kurekodiwa.
  • Uwekezaji barani uropa uliongezeka kwa asili mia 39 na kufikia dola za Marekani bilioni 61.2

Frankfurt/Nairobi, 18 June 2019 –Uwekezaji ulimwenguni katika nishati jadidifu ulifikia dola za marekani bilioni 288.9 katika mwaka wa 2018, na fedha zilizotumika kwa vifaa vipya zikizidi gharama za kifedha za nishati mpya ya mafuta ya gesi. Hii ni kwa mujibu wa takwimu mpya zilizochapishwa leo.

Takwimu hizi, zilizotolewa na BloombergNEF (BNEF), zinachapishwa leo kama sehemu ya ripoti ya kimataifa ya REN21’s Renewables 2019 Global Status Report.

Takwimu zinaonyesha kuwa ijapokuwa uwekezaji ulipungua katika kipindi cha mwaka uliopita, mwaka wa 2018 ulikuwa mwaka wa tisa mtawalia ambapo uwekezaji ulikuwa zaidi ya dola za Marekani bilioni 200 na mwaka wa tano mtawalia kufikia zaidi dola za Marekani bilioni 250. Takwimu hazijajumuisha umeme wa nguvu za maji wa zaidi ya mega wati 50, uliopokea uwekezaji wa zaidi ya dola za Marekani bilioni 16- ukiwa pia kidogo kuliko mwaka wa 2017, ambapo dola za Marekani bilioni 40 ziliekezwa.

Kupungua kwa uwekezaji katika mwaka wa 2018 kwa kiwango fulani kunaweza kuhusishwa na kupungua kwa bei ya teknolojia ya vizio vya nguvu za umeme zitokanazo na jua. Hii  ilimaanisha kuwa kiwango kilichohitajika kingepatikana kwa bei nafuu, na kwa hivyo kupunguza gharama ya uwekazaji wa nishati ya jua nchini China.

Hata hivyo, katika ngazi ya kimaataifa, nishati ya jua ilipokea uwekezaji mkubwa, kwa dola za Marekani bilioni 139.7 katika mwaka wa 2018, ikipungua kwa asili mia 22. Uwekezaji katika nishati ya upepo uliongezeka kwa asili mia mbili katika mwaka wa 2018 na kufikia dola za Marekani bilioni 134.1. Sekta nyingine zilisalia nyuma sana ijapokuwa uwekezaji katika maeneo ya viumbe hai na kutengeneza nishati kutoka kwa taka kuliongezeka kwa asili mia 54 na kufikia dola za Marekani bilioni 8.7.

Takwimu hizo zinalingana na kiwango cha uwekezaji uliofanywa kwa vifaa vipya vya nishati jadidifu, ambao ulifikia dola za Marekani bilioni 272.3 kwenye kiwango cha kimataifa katika mwaka wa 2018 (bila kujumuisha haidro kubwa), ikiwa ni pamoja na uwezo wa kupata nishati kutoka kwa makaa ya mawe na gesi, ambayo ilikuwa dola za Marekani bilioni 95.

"Mielekeo ya kimataifa inaendelea kuonyesha kwamba kuwekeza kwa nishati jadidifu ni kuwekeza kwa manufaa ya siku zijazo. Uwekezaji kwenye nishati jadidifu katika mwaka wa 2018 uliimarika mara tatu zaidi ikilinganishwa na kiwango kilichoekezwa kwenye genereta mpya zinazotumia makaa ya mawe na gesi," alisema Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP). "Ijapokuwa hali hii inatia moyo, tunapaswa kuongeza mwendo kwa kasi iwapo tuna nia ya kufikia malengo ya tabia nchi na ya maendeleo ya kimataifa."

China yaongoza huku ikifuatiwa na uropa na nchi zinazoendelea

Tukigawa kwa maeneo ya kijiografia jumla ya dola za Marekani bilioni 288.8 zilizotumika katika uwekezaji wa nishati jadidifu katika mwaka wa 2018, inaonyesha China iliongoza kwa uwekezaji duniani kwa miaka saba mtawalia, kwa dola za Marekani bilioni 91.2. Hata hivyo, ulipungua kwa asili mia 37 ikilinganishwa na mwaka wa 2017 kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kubadilishwa kwa sera ya serikali inayopendelea nishati jadidifu katikati ya mwaka, hali ilioathiri nishati ya jua.

China pia iligharamia asili mia 32 ya jumla ya uwekezaji duniani, huku ikifuatiwa na uropa kwa asili mia 21, Marekani kwa asili mia 17 na Asia-Oceania (bila kujumuisha China na India) kwa asili mia 15. Kiwango cha chini kilishuhudiwa India kwa asili mia 5, Mashariki ya Kati na Africa kwa asili mia 5, Waamerika (bila kujumuisha Brazil na Marekani) kwa asili mia 3 na Brazil kwa asili mia 1.

Bila kujumuisha China, uwekezaji katika nishati jadidifu katika nchi zinazoendelea uluongezeka hasa kwa asili mia 6 na kufikia dola za Marekani bilioni 61.6, ikiwa ni kiwango cha juu kuwahi kerekodiwa.

"Wakati ambapo uwekezaji kwa jumla unapungua, ni rahisi kufikiria tunarudi nyuma, lakini sivyo," Angus McCrone, Mhariri Mkuu katika BloombergNEF, alisema: "Nishati jadidifu inaendelea kupungua bei na tunashuhudia ongezeko la uwekezaji kwenye upepo na jua katika nchi zaidi kule Asia, Mashariki ya Uropa, Mashariki ya Kati na Afrika."

Uwekezaji barani uropa uliongezeka kwa asili mia 39 na kufikia dola za Marekani bilioni 61.2, ambacho ni kiwango cha juu sana kwa kipindi cha miaka miwili, ikichangiwa pakubwa na uwekezaji mkubwa kwa upepo kutoka karibu na mbali ya bahari.

Marekani, uwekezaji uliongezeka kwa asili mia 1 na kufikia dola za Marekani bilioni 48.5, kiwango cha juu zaidi tangu mwaka wa 2011, pia ikichangiwa na ongezeko la uwekezaji kwenye nishati ya upepo.

Uwekezaji katika eneo la  Asia ya Pasifiki (bila kujumuisha China na India) uliongezeka kwa asili mia 6 na kufikia dola za Marekani bilioni 44.2, kiwango cha juu zaidi kwa miaka mitatu, na Mashariki ya Kati na Afrika zilishuhudia ungezeko la asili mia 57 na kuandikisha rekodi ya dola za Marekani bilioni 15.4. Hata hivyo, kwa Waamerika (bila kujumuisha Brazil na Marekani), uwekezaji ulipungua kwa asili mia 23 (bila kujumuisha umeme wa nguvu za maji) na kufikia dola za Marekani bilioni 9.8. 

"Ni jambo linalotia moyo kuona uwekezaji ukiongezeka Marekani," alisema Dakt. Prof. Nils Stieglitz Rais wa Taasisi ya Fedha na Menejimenti (Frankfurt School of Finance & Management), mhusika kwa ripoti hiyo, "Kinyume na matarajio, ongezeko la uwekezaji katika kawi jadidifu unaweza kuchangiwa na miradi iliyo mbioni kunufaika na mpango uliopo wa kodi unaopenendelea nishati jadidifu, ambao utafika mwisho katika miaka michache tu ijayo kwa sababu uwezekano wa koungeza mda wake wa matumizi ni mdogo mno."

Taarifa zaidi na kwa mapana katika uwekezaji ulimwenguni hasa kufadhili nishati jadidifu katika mwaka wa 2018 itawekwa kwenye chapisho la Global Trends in Renewable Energy Investment report, litakalotolewa Septemba kabla ya mkutano mkuu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa unaojishughulisha na tabia nchi ulimwenguni ( the Global Climate Action summit of the UN Secretary-General). Ripoti hii huchapishwa kila mwaka tangu mwaka wa 2007. Toleo la mwaka huu limefadhiliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Mazingira ya Ujerumani (German Federal Ministry for the Environment), na Shirika la Utunzaji wa Mali Asili na Usalama wa Nyuklia (Nature Conservation and Nuclear Safety). Itaonyesha uwekezaji kwa nishati jadidifu kwa muongo mmoja uliopita.

MAKALA KWA MHARIRI

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa

Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa ndilo sauti kuu ya kimataifa kuhusu mazingira. Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika kutunza mazingira kupitia kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo. Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa hufanya kazi pamoja na serikali, sekta ya kibinafsi, mashirika ya uraia na Taasis zinginezo za Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa kote ulimwenguni.

Kuhusu Taasis ya Frankfurt School na Kituo cha Frankfurt School-UNEP Centre

Taasis ya Frankfurt School – UNEP Collaborating Centre for Climate & Sustainable Energy Finance ina ushirikiano kutoka kwaTaasis ya Frankfurt School of Finance & Management na Shirika la Mazingira la Umoja wa mataifa. Kituo hiki kimejitolea kuleta mabadiliko yanayohitajika katika usambasaji wa kawi na matumizi yake kote ulimwenguni kwa kusaidia sekta za kibinafsi kifedha kuwekeza katika nishati endelevu  na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Kwa taarifa zaidi

Keishamaza Rukikaire, Mkuu wa Habari na Vyombo vya Habari, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa

Jennifer Pollak, Frankfurt School of Finance & Management