10 Jul 2019 Toleo la habari Youth, education & environment

Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Ngazi ya Juu kote duniani zatangaza udharura wa kushughulikia tabia nchi.

New York, 10 Julai 2019 - Leo, mitandao inayoleta pamoja Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya juu zaidi ya 7,000 kutoka kwa mabara yote 7, ilitangaza ya kuwa kuna udharura wa kushughulikia tabia nchi. Walikubaliana kutoa utaratibu ulio na vipengele vitatu wa kukabiliana na janga hilo kupitia kazi yao na wanafunzi.

Utaratibu ulio na vipengele vitatu ni pamoja na:

1. Kujitolea kuepukana na hewa ya ukaa ifikiapo 2030 au 2050 ikilazimu;

2. Kutafuta rasilimali zaidi ili kufanya utafiti wa kuleta suluhisho kwa mabadiliko ya tabia nchi na kubuni maarifa mapya;

3. Kuongeza utoaji wa elimu kuhusu mazingira na kuifanya iwe endelevu kupitia kwa mitaala na programu za uhamasishaji katika vyuo na katika jamii.

Barua, iliyoandaliwa na 'The Alliance for Sustainability Leadership in Education', inayofahamika kama EAUC, shirika lenye makao yake makuu Marekani la taasisi za elimu ya ngazi ya juu linaloshughulikia masuala ya tabia nchi, Second Nature, na Youth and Education Alliance ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa. Ni mara ya kwanza kwa vyuo na taasisi za elimu ya ngazi ya juu kukuja pamoja kujitolea kushirikiana kwa kukubali kuna udharura wa kushughulikia tabia nchi. Itasomwa New York katika mkutano wa mawaziri wa Mradi Endelevu wa Taasisi za Elimu ya Juu.

Ilitiwa sahihi na vyuo vikuu ambavyo ni pamoja na Chuo Kikuu cha Strathmore (Kenya), Chuo Kikuu cha Tongji (China), KEDGE Business School (Ufaransa), Chuo Kikuu cha Glasgow (UK), Chuo Kikuu cha California State University (USA), Chuo Kikuu cha Zayed (UAE) na Chuo Kikuu cha Guadalajara (Mexico), mwito huu pia unaungwa mkono na Global Alliance na the Globally Responsible Leadership Initiative, ambo wamejitolea kuwa matafikia malengo yaliyopendekezwa ya kuepukana na hewa ya ukaa.

Tunayoyafundisha sasa yanatoa mwelekeo kwa siku sijazo. Tunakaribisha kujitolea huku kwa Vyuo kwa kutoathiri tabia nchi ifikiapo 2030 na kuimarisha juhudi zao vyuoni,” alisema Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa,. "Kuna ongezeko la vijana walio katika mstari wa mbele wa kutoa mwito wa kukabiliana na changamoto zinakabili tabia nchi na mazingira. Miradi inayoshirikisha vijana moja kwa moja katika kazi hii muhimu ni mchango mkubwa kwa juhudi za kimataifa za kuwa na mazingira endelevu."

Mifano ya kazi nzuri ya kupigiwa upato vyuoni inajumuisha Chuo Kikuu cha Strathmore kutoka Kenya, kinachoendeshwa kwa kutumia nishati safi na kina mfumo wake wa gridi ya kupata umeme kutokana na mwanga wa kilowati 600, na Chuo Kikuu cha Tongji kilichoko Uchina, ambacho kimeekeza mno katika mtaala endelevu wa elimu na kinahimiza taasisi zingine za elimu kufanya hivyo. Kule Marekani, Chuo Kikuu cha California kimejitolea kutimiza lengo kuu la mfumo wake wa kuepukana na hewa ya ukaa ifikiapo 2025, na wengine, kama vile Chuo Kikuu cha Amerika na Chuo Kikuu cha Colgate, wameepukana kabisa na hewa ya ukaa.

Akiunga mkono juhudi hizo, Charlotte Bonner, Mkurugenzi wa Wanafunzi Wanaoandaa Kuwepo kwa Uendelevu (Students Organizing for Sustainability) alisema: "Vijana kutoka sehemu mbalimbali za ulimwengu wanahisi kuwa shule, vyuo na vyuo vikuu havijaharakisha kushughulikia janga ambalo linatuathiri sasa. Tunapokea kwa furaha taarifa kuwa wanatangaza kuna haja ya kuwa na udahrura wa kushughulikia tabia nchi. Hatuna mda wa kupoteza. Tunatoa wito kwa wale ambao bado hawajajiunga na mradi huu, wajiunge na wenzao. Bila shaka, swala la muhimu mno ni yale yatakayofuatia."

Matarajio ni kuwa zaidi ya taasisi 10,000 za elimu ya juu na vyuo vitajiunga kabla ya mwisho wa mwaka wa 2019, huku serikali zikialikwa kusaidia viongozi wao kwa kuwatunuku ili kufanya kazi.

TAARIFA KWA WAHARIRI

Soma barua nzima na uone Mitandao ambayo imetia sahihi kuonyesha zimejitolea

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa

UNEP ni msemaji mkubwa wa kimataifa kuhusu mazingira. Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika kutunza mazingira kupitia kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo. UNEP hufanya kazi pamoja na serikali, sekta ya kibinafsi, mashirika ya uraia na Taasis zinginezo za Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa kote ulimwenguni.

Kuhusu EAUC

EAUC ni muungano wa uongozi endelevu kwenye sekta ya elimu. EAUC ina wawakilishi kutoka taasisi 200 zilizo na jumla ya wanafunzi milioni 2 na wafanyikazi wapatao 400,000 na bajeti yao ya matumizi huwa Pauni bilioni 25. Sisi huwasaidia viongozi, walimu na wanafunzi katika taasis za elimu na wataalamu kudumisha uendelevu katika taasisi 16 za elimu ya ngazi ya juu. Vyuo vikuu na vyuo endelevu hufaulu mno kwa kipindi kirefu. Vyuo hivyo hupata fedha zaidi na kufanya kazi kwa udhabiti, huwa na matokeo bora kutoka kwa wanafunzi, huathiri jamii mno na kuwa na utafiti na ubunifu duniani.

Kuhusu Second Nature

Second Nature imejitolea kushughulikia mazingira kupitia taasisi za elimu ya ngazi ya juu. Haya hufanyika kupitia kwa kuhimiza taasisi nyingi za elimu ya ngazi ya juu kujitolea kushughulikia mazingira kikamilifu, kuanzisha miradi vyuoni, na kutoa masuluhisho ya kukabiliana na tabia nchi kupitia ubunifu. Second Nature inalenga kuleta pamoja, kuimarisha na kuchangia katika juhudi za sekta kwa ushirikiano na viongozi wa kimataifa ili kushughulikia tabia nchi kwa dharura.

Kwa maelezo zaidi, wasiliana na:

Keishamaza Rukikaire, Msimamizi wa Habari na Vyombo vya Habari,, UNEP +254 722677747