Pixabay
04 Nov 2021 Toleo la habari Kushughulikia Mazingira

Imarisha juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi au mkabiliane na changamoto kubwa: Ripoti ya UN

  • Makadirio ya gharama za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika nchi zinazoendelea ni kubwa mara tano hadi kumi zaidi kuliko mtiririko wa sasa wa fedha za umma za kukabiliana na gesi chafu. 
  • Chini ya theluthi moja ya nchi 66 zimefadhili wazi mikakati ya kukabiliana na COVID-19 ili kushughulikia madhara kwa mazingira.
  • Zaidi ya miradi 2600 inaangazia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

 

Glasgow, Novemba 4, 2021 – Wakati mataifa yanapokusanyika kujadiliana kuhusu mazingira mjini Glasgow, ripoti mpya ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) imetoa wito wa kufanya juhudi kwa dharura kuimarisha ufadhili na utekelezaji wa hatua za kukabiliana na athari zinazozidi kuongezeka zaya mabadiliko ya tabianchi.

Ripoti ya Kukabiliana na Pengo la Uzalishaji wa Gesi Chafu ya Mwaka wa 2021: Dhoruba Inajikusanya inaonyesha kuwa ijapokuwa sera na mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi inaongezeka, ufadhili na utekelezaji wake bado hautoshi.

Kwa kuongezea, ripoti hii inaonyesha kuwa fursa ya kutumia bajeti ya kujikwamua na janga kutoa kipaumbele kwa juhudi zinazokuza uchumi bila kuchafua mazingira na kuwezesha kustahimili athari za mabadiliko ya tabianchi kama vile ukame, dhoruba na mioto msituni inaendelea kupotea.

“Wakati dunia inapoweka juhudi za kupunguza uzalishaji wa gesi chafu - juhudi ambazo bado hazitoshi - ni lazima pia iimarishe kwa kasi juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi,” amesema Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP. "Hata kama tungesitisha uzalishaji wa gesi ya uka leo, athari za mabadiliko ya tabianchi zitasalia nasi kwa miongo mingi ijayo. Tunahitaji hatua za kubadilisha ahadi za ufadhili na utekelezaji ili kupunguza kwa kiasi kikubwa uharibifu na hasara zanazotokana na mabadiliko ya tabianchi. Na tunaihitaji kufanya hivyo sasa.”

Ufadhili wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ni dhaifu

Ahadi za sasa chini ya Mkataba wa Paris zinaonyesha kutakuwa na ongezeko la joto la nyuzijoto 2.7 duniani kufikia mwishoni mwa karne hii. Hata dunia ikidhibiti ongezeko la joto lisizidi nyuzijoto 1.5 au nyuzijoto 2, kama ilivyoainishwa kwenye mkataba, bado kuna hatari nyingi kwa mazingira.  Ijapokuwa upunguzaji mkuu ndio njia mwafaka zaidi ya kupunguza athari na gharama za mda mrefu, kuimarisha ahadi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, hasa ufadhili na utekelezaji ni muhimu ili kuzuia mapengo yaliyopo yasiongezeke.

Ripoti hii inaonyesha kuwa gharama za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi huenda zikaongezeka na kukadiriwa kufikia dola za Marekani kati ya bilioni 140 na bilioni 300 kwa mwaka kufikia mwaka wa 2030 na dola za Marekani kati ya bilioni 280 na bilioni 500 kwa mwaka kufikia mwaka wa 2050 kwa nchi zinazoendelea pekee. Ufadhali wa mazingira unaofanywa katika nchi zinazoendelea ili kuweka na kutekeleza mikakati ya kukabiliana na gesi chafu zilifikia dola za Marekani bilioni 79.6 katika mwaka wa 2019. Kwa jumla, makadirio ya gharama za kukabiliana na gesi chafu katika nchi zinazoendelea ni kubwa mara tano hadi kumi zaidi kuliko mtiririko wa sasa wa fedha za umma za kukabiliana na gesi chafu, na pengo hili linazidi kuongezeka.

Fursa ya COVID-19 inaendelea kupotea

Dola za Marekani trilioni 16.7 za bajeti kote ulimwenguni zimetengewa kukabiliana na hali hiyo. Lakini ni sehemu ndogo tu ya fedha hizi zimetengewa kukabiliana na gesi chafu. Chini ya theluthi moja ya nchi 66 zilizofanyiwa utafiti zimefadhili wazi mikakati ya kukabiliana na COVID-19 ili kushughulikia mabadiliko ya tabianchi kufikia Juni mwaka wa 2021. Wakati uo huo, gharama ya juu ya kulipa madeni ikijumuishwa na ukusanyaji wa ushuru uliopungua, vinaweza matumuzi ya baadaye ya serikali ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, hasa katika nchi zinazoendelea.

Kuna hatua za mikakati na utekelezaji

Ijapokuwa ushahidi wa mapema unaonyesha kuwa Mikakati ya Kitaifa ya Kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi imeathiriwa na COVID-19, hatua zinapigwa kuhusiana na ajenda za kitaifa za kukabiliana na gwsi chafu.

Takribani asilimia 79 ya nchi zimepitisha angalau mkakati mmoja wa kitaifa wa kukabiliana na gesi chafu, kama vile mpango, mkakati, sera au sheria.  Hili ni ongezeko la asilimia saba tangu mwaka wa 2020.

Asilimia tisa ya nchi ambazo hazina mkakati wa aina hii zimeanza kuweka. Takribani asilimia 65 ya nchi zina mkakati mmoja au zaidi wa kisekta na angalau asilimia 26 tu ya nchi zina mkakati mmoja au zaidi katika eneo ndani ya nchi.

Hata hivyo, utekelezaji wa hatua za kukabiliana na gesi chafu unaendelea kuongezeka polepole. Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD) linaonyesha kuwa wafadhili kumi wakuu walifadhili zaidi ya miradi 2,600 inayolenga kukabiliana na uzalishaji wa gesi chafu kati ya mwaka wa 2010 na mwaka wa 2019. Miradi inazidi kuimarika, huku mingi ikivutia ufadhili zaidi ya dola za Marekani milioni 10.

Juhudi zaidi zinahitajika

Licha ya mafanikio fulani, juhudi zaidi zinahitajika za kufadhili na kuwezesha utekelezaji.

Dunia inapaswa kuimarisha ufadhili wa umma wa kukabiliana na gesi chafu, kupitia uwekezaji wa moja kwa moja na kwa kukabiliana na vikwazo vya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika sekta binafsi. Utekelezaji wa hatua dhabiti zaidi za kukabiliana na gesi chafu unahitajika ili kuepuka kushindwa kudhibiti madhara kwa mazingira, hasa katika nchi zinazoendelea. Ulimwengu pia unahitaji kuzingatia majanga mabaya kabisa kwa mazingira yanayoangaziwa na Ripoti ya Sita ya Tathmini ya Jopo la Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi.

Ripoti hiyo pia ilionyesha kuwa serikali zinapaswa kutumia bajeti ya kujikwamua na janga kutoa kipaumbele kwa juhudi zinazokuza uchumi na kuwezesha kustahimili mabadiliko ya tabianchi. Zinapaswa kuanzisha mifumo ya ufadhili wa kushughulikia majanga inayoweza kubadilika. Nchi zilizoendelea zinapaswa kusaidia nchi zinazoendelea na fedha ili kuziwezesha kujiimarisha bila kuchafua mazingira baada ya COVID-19 kwa kuzipa fedha kwa masharti nafuu na kuzisamahe madeni makuu.

 

MAKALA KWA WAHARIRI

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP)

UNEP ni mhamasishaji mkubwa wa masuala ya mazingira kote duniani. Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano wa utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.

Kwa taarifa zaidi tafadhali waliliana na:

Keisha Rukikaire, Mkuu wa Habari na Vyombo vya Habari, Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa