Pixabay
09 Dec 2020 Toleo la habari Kushughulikia Mazingira

Kuimarisha uchumi bila kuchafua mazingira ni muhimu ili kupunguza pengo la kushughulikia mazingira- Ripoti ya UN

  • Kuimarisha uchumi bila kuchafua mazingira kunaweza kudhibiti kiwango cha joto na kukifanya kuwa karibu ya kile kinachohitajika cha nyuzijoto 2, na hata kuweka juhudi zaidi hadi kufia nyuzijoto 1.5 zinazolengwa
  • Kupunguka kwa uzalishaji wa gesi chafu kwa asilimia 7 katika mwaka wa 2020 hakutakuwa na athari kubwa kwa mabadiliko ya tabianchi 
  • Ahadi za kutozalisha gesi ya ukaa zinakaribishwa, ila serikali zinapaswa kudhihirisha kujitolea kwake kupitia ahadi zilizotolewa chini ya Mkataba wa Paris na kuchukua hatua dhabiti 

 Nairobi, Disemba 9, 2020 – Kuimarisha uchumi bila kuchafua mazingira kunaweza kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa kwa asilimia 25 kutoka kwa ile inayotabiriwa kufikia mwaka wa 2030 na kuifanya dunia kuwa karibu kufikia lengo la nyuzijoto 2 kama ilivyo kwenye Mkataba wa Paris wa Mabadiliko ya tabianchi, matokeo ya ripoti mpya ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) yaonyesha.

Matokeo ya Ripoti ya UNEP inayotolewa kila mwaka ya Emissions Gap Report 2020  inaonyesha kuwa ijapokuwa kumekuwa na upunguzaji wa uzalishaji wa kaboniksidi katika mwaka wa 2020 kutokana na janga la korona (COVID-19), ongezeko la joto duniani linaelekea kuwa juu zaidi kwa nyuzijoto 3 katika karne hii.

Hata hivyo, iwapo serikali zitawekeza kwenye utunzaji wa mazingira kama sehemu ya kujimairisha baada ya janga la korona na kuimarisha ahadi za kutozalisha gesi ya ukaa na kutoa ahadi zaidi wakati wa mkutano ujao wsa mazingira– utakaotokea mjini Glasgow mwaka wa 2021 – zinawezafikia lengo la kudhibiti kiwango cha joto kuwa nyuzijoto 2.

Kwa kujumuisha juhudi za kutochafua mazingira wakati wa kujiimarisha baada ya korona na hatua za dharura za kujumuisha ahadi za kutozalisha gesi ya ukaa kwenye ahadi zitakazotolewa upya na taifa (NDCs) chini ya Mkataba wa Paris, na kufuatia na hatua dhabiti zitakazochukuliwa kwa dharura, serikali bado zinaweza kufikia lengo la nyuzijoto 1.5.

“Kiwango cha joto kilikuwa juu zaidi katika mwaka wa 2020 huku madhara ya mioto maporini, dhoruba na kiangazi yakiendelea kushuhudiwa," alisema Inger Andersen, Katibu Mtendaji wa UNEP. "Hata hivyo, Ripoti ya UNEP ya Emissions Gap inaonyesha kuwa kujumuisha juhudi za kutochafua mazingira wakati wa kujiimarisha baada ya korona kunaweza kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa na kupunguza mabadiliko ya tabianchi. Natoa wito kwa serikali kutumia nishati isiyochafua mazingira zinapojiimarisha baada ya korona (COVID-19) na kuimarisha ahadi zake mno katika mwaka wa 2021”

Kila mwaka, Ripoti ya Emissions Gap hutathmini pengo kubwa lililopo kati ya viwango vya uzalishaji wa gesi chafu vinavyokusudiwa na viwango vinavyopatikana kwenye malengo ya Mkataba wa Paris ya kudhibiti ongezeko la joto katika karne hii visizidi nyuzijoto 2 na kuendelea kutafuta kufikia nyuzijoto 1.5. Ripoti hii inaonyesha kuwa katika mwaka wa 2019 uzalishaji wa gesi ya ukaa kwa jumla, ikijumuisha mabadiliko katika matumizi ya ardhi, iliongezeka na kufikia gigatani za kaboniksidi (GtCO2e) 59.1. Uzalishaji wa gesi ya ukaa duniani umeongezeka kwa wastani ya asilimia 1.4 kwa mwaka tangu mwaka wa 2010, Kiwango kikubwa cha asilimia 2.6 kikishuhudiwa katika mwaka wa 2019 kutokana na ongezeko la mioto misutuni.

Kutokana na kupungua kwa safari, shughuli zilizopungua katika viwanda na uzalishaji mdogo wa umeme katika mwaka huu kutokana na janga la korona, uzalishaji wa kabonikisidi unatarajiwa kupungua kwa asilimia 7 katika mwaka wa 2020.  Hata hivyo, hii inamaanishi kuwa ongezeko la joto duniani litapungua tu kwa asilimia 0.01 kufikia mwaka wa 2050. Kwa sasa, NDCs hazijatosha.

Ni muhimu kuimarisha uchumi bila kuchafua mazingira

Kuimarisha uchumi bila kuchafua mazingira hata hivyo, kunaweza kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa kwa asilimia 25 kutoka kwa ile inayotabiriwa kufikia mwaka wa 2030 kwa kuzingatia sera zilizokuwepo kabla ya COVID-19. Kujiimarisha kwa kutochafua mazingira kunaweza kufanya uzalishaji wa gesi chafuzi katika mwaka wa 2030 kuwa GtCO2e 44 badala ya GtCO2e 59 zilizotabiriwa– kuliko kiwango cha upunguzaji kwa kuzingatia ahadi zinazotolewa kwa hiari za NDCs, hali itakayopelekea ongezeko la joto duniani kufikia nyuzijoto 3.2.

Kujiimarisha kwa kutochafua mazingira kwa namna hii kunaweza kufanya kuwepo na uwezekano wa asilimia 66 wa kudhibiti kiwango cha joto kuwa chini ya nyuzijoto 2, ila haitawezekana kufikia lengo la nyuzijoto 1.5.

Hatua zinazopaswa kuchukuliwa kwa haraka zinajumuisha kuunga mkono matumizi ya teknolojia na miundo msingi zisizozalisha gesi ya ukaa, kupunguza ruzuku inayotolewa kwa nishati ya visukuku, kutoruhusu viwanda vipya vya mawe ya makaa, na kutoa masuluhisho yanayojali mazingira – ikijumuisha kuboresha kiwango kikubwa cha ardhi na kupanda miti katika maeneo iliyokatwa

Kufika sasa, ripoti hiyo inaonyesha kuwa bajeti iliyotengewa juhudi za kuimarisha uchumi bila kuchafua mazingira ni ndogo. Takribani robo ya nchi wanachama wa G20 zimetenga fungu la pesa za matumizi la asilimia 3 ya Pato la Taifa (GDP), kuwezesha mikakati ya kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa. 

Hata hivyo, bado kuna fursa kubwa kwa nchi kutekeleza sera na miradi isiyozalisha gesi ya ukaa.  Serikali zinapaswa kutumia fursa hii wakati zinapochukua hatua za kukabiliana na korona zinapounda bajeti, kwa mjibu ya ripoti hiyo.   

Matokeo ya ripoti hiyo pia yanaonesha kuwa idadi inayoendelea kuongezeka ya nchi zinazotoa ahadi ya kutozalisha  gesi ya ukaa kufikia nusu ya karne hii ni "suala nyeti linalostahili kupigiwa upato". Wakati ripoti hiyo ilipokamilishwa, nchi 126 zinazokadiria asilimia 51 ya uzalishaji wa gesi ya ukaa duniani, zimeidhinisha, kutangaza au kuweka malengo ya kutozalisha gesi hiyo.

Hata hivyo, ili kufaulu na kutekelezeka, ahadi hizi zinapaswa kufanyiwa kazi upesi ili kuunda sera na kuchukua hatua kwa dharura inavyojitokeza kwenye NDCs. Ahadi za kipekee kwenye Mkataba wa Paris zinahitaji kuimarishwa mara tatu zaidi ili kufikia nzuzijoto 2 na kuimarishwa angalau mara tano zaidi ili kufikia nyuzijoto 1.5.

Ni muhimu kubadili mienendo ya matumizi ya bidhaa

Kila mwaka, ripoti hiyo pia huangazia uwezo kwenye sekta maalum. Katika mwaka wa 2020, inaangazia mienendo ya watu kwenye sekta ya usafiri wa meli na wa ndege.

Sekta za usafiri wa meli na wa ndege, zinazochangia asilimia 5 ya uzalishaji wa gesi chafu duniani, pia znahitaji kushughulikiwa. Kuimarishwa kwa teknolojia na utendakazi kunaweza kuimarisha ubora wa nishati inayotumiwa kwa usafiri iwapo matuzo yatatolewa. Ila, ongezeko linalokisiwa kutokea inamainisha kuwa gesi ya ukaa wala kabonikisidi havitapungua.  Sekta hizo zinapaswa kutumia nishati itakayoziwezesha kuepukana na nishati ya visukuku

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa hatua dhabiti za kushughulikia mazingira zinapaswa kujumuisha mabadiliko ya jinsi ya kutumia bidhaa kwenye sekta binafsi na ya mienendo ya watu binafsi. Takribani thuluthi mbili za uzalishaji wa gesi chafu hutoka kwa majumba yanayomilikiwa na watu binafsi, kwa kuzingatia data ya matumizi ya bidhaa. 

Watu wakwasi wanapaswa kuwajibika zaidi: uzalishaji wa watu wote matajiri zaidi ambao ni asilimia moja ya idadi ya watu wote duniani hukadiria zaidi ya maradufu ya uzalishaji ikilinganishwa na wa asilimia 50 ya watu maskini zaidi.  Matajiri wanapaswa kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa angalau mara 30 zaidi ili kuwezesha kufikia malengo ya Paris. 

Juhudi zinazoweza kusaidia kuepukana na bidhaa zilizo na kiwango cha juu cha gesi ya ukaa ni pamoja na kutumia magarimoshi badala ya kutumia ndege kwa safari fupi, matuzo na miundo msingi ili kuwezesha matumizi ya baisikeli na watu kutumia magari yao na wenzao, kuboresha nishati inayotumika majumbani, na sera za kupunguza uharibifu wa chakula.

MAKALA KWA WAHARIRI

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa

UNEP ni mhamasishaji mkubwa wa masuala ya mazingira duniani.   Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo. 

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:

Keisha Rukikaire, Msimamizi wa Habari na Vyombo vya Habari, UNEP, +254 722 677747, rukikaire@un.org