05 Aug 2020 Toleo la habari Vichimbuaji

Viwango Vipya vya Kimataifa vya Usimamizi wa Sekta ya Uchimbaji wa Madini vinalenga kuimarisha usalama katika vituo vya uchimbaji wa madini…

Agosti 5, 2020, London – Viwango vya Kimataifa vya Usimamizi wa Sekta ya Uchimbaji wa Madini (the Standard) vilivyozinduliwa leo, ni vya kwanza katika ngazi ya kimataifa vinavyoweza kutumika kwa sasa na kwa siku zijazo kushughulikia vituo vya uchimbaji wa madini popote viliopo na wanaofanya kazi huko.

Vimeimarisha juhudi zilizopo katika sekta ya uchimbaji wa migodi kwa kuongezea vipengele vya mazingira, vya kijamii, vya uchumi wa maeneo husika, na vya kiufundi. Viwango hivyo vinahusu mchakato mzima wa uchimbaji wa madini-kuanzia kwa kuchagua eneo, miundo na ujenzi, usimamizi na ufuatiliaji hadi ufungaji wake na yanayotokea baada ya ufungaji.

Kwa lengo la kutosababisha madhara yoyote kwa binadamu na kwa mazingira, Viwango hivyo vinaimarisha juhudi za sekta hiyo kuwa na matokeo mazuri ya kijamii, kwa mazingira na ya kiufundi. Vinaimarisha uwajibikaji wa kiwango cha juu na kuweka masharti mapya kuhusu maoni ya watu binafsi. Viwango hivyo pia vinaweka wazi matarajio mapya kote ulimwenguni ya kufanya kazi kwa njia ya wazi na ya kujitolea, hali itakayoboresha uelewa wa wadau ambao wangependa kuwekeza katika sekta hiyo.

Viwango hivyo vimewekwa kupitia mchakato wa kujitegemea –  Global Tailings Review (GTR) –iliyowekwa mnamo Machi mwaka wa 2019 kwa ushirikiano na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Kanuni za Uwekezaji Mwafaka (PRI) na Baraza la Kimataifa la Uchimbaji wa Mikodi na Madini (ICMM) kufuatia maporomoko mabaya yaliyotokea Brumadinho, nchini Brazil, tarehe 25 Januari, 2019.

Watu wote walioshirikiana kuandaa wameidhinisha na wanatoa wito wa utekelezaji wake mkubwa katika sekta hiyo: 

  • UNEP itasaidia serikali zinazotaka kuvitumia na kuongeza kwa sheria na sera zake za kitaifa au za majimbo.
  • PRI, inayowakiisha dola trilioni 103.4 za Marekani za mali inayosimamiwa itaboresha matarajio ya wawekezaji ya kusaidia kampuni zote za uchimbaji migodi kutekeleza Viwango hivyo.
  • Kampuni wanachama wa ICMM zitatekeleza Viwango hivyo kama sehemu ya kuwa wanachama waliojitolea. Hii ni pamoja na udhibitishaji wa maeneo ya machimbo na tathmini kutoka kwa watu wasiohusika moja kwa moja. 

Dr Bruno Oberle, mwenyekiti wa Global Tailings Review alisema: "Tuna furaha isiyokuwa na kifani kuzindua Viwango vya Kimataifa vya Usimamizi wa Sekta ya Uchimbaji wa Madini, ambao ni mwanzo wa usimamiaji mzuri wa vituo vya uchimbaji wa madini na kuvifanya kutodhuru maisha ya yeyote.

"Maporomoko mabaya mno ya bwawa katika eneo la migodi la Vale’s Córrego de Feijão, Brumadinho ulikuwa mkasa kwa binadamu na kwa mazingira uliotaka hatua za kuimarisha usalama na kuimarisha usimamiaji wa vituo vya uchimbaji wa madini kote duniani kuchukuliwa. Hasa, nina furaha isiyokuwa na kifani kuwa na makala yanayoangazia na kushughulikia changamoto changamano na kutoa suhulu linalokata ndani ya sekta mbalimbali la kusimamia vituo vya uchimbaji madini ipasavyo.

"Nilitunukiwa fursa ya kusimamia kazi hii na sasa natoa wito kwa kampuni zote za uchimbaji wa migodi, serikali na wawekezaji kutumia Viwango hivi na kuendelea kufanya kazi pamoja ili kuimarisha vituo vya uchimbaji wa madini kote duniani. Ni matumaini yangu kuwa Viwango hivi vitaungwa mkono na mashirika yanayojitegemea ili kudumisha ubora wake na hata kuviboresha zaidi mda unapoendelea kusonga."

Ligia Noronha, Mkurugenzi wa Kitengo cha Masuala ya Uchumi cha UNEP alisema: "Vituo vya uchimbaji wa madini ni sharti vizingatie usalama kwanza kwa kutoa kipao mbele kwa usalama wa mazingira na usalama wa binadamu katika hatua za usimamiaji na utendakazi wake. Viwango vya Kimataifa vya Usimamizi wa Sekta ya Uchimbaji wa Madini ni idhibati ya hatua muhimu za kuwezesha kutokuwepo na madhara yoyote kwa binadamu na kwa mazingira kutoka kwa vituo vya uchimbaji wa madini. Athari zake zitategemea uktelezaji wake na UNEP itaendelea kushiriki katika utekelezaji wake. Tunashauriwa na  kujitolea na majukumu ya ICMM kuhusu utekelezaji wa Viwango ivyo na kutoa wito kwa kekta ya madini, na wale wanaoifadhili na kuwekeza katika sekta hiyo kujitolea pia. Ili kudumisha uwajibikiaji wa Viwango hivyo, ni muhimu kwa mashirika yasihusika katika sekta hiyo kubainisha na kufuatilia utekelezaji wa vitu kama vile uundaji wa taasisi zinazojitegemea. Kufikia hapa, UNEP itaendelea kushauriana na wadau wengine walio na nia ya kupata suluhu."

Adam Matthews, Kikosi cha Maadii, Uwajibikaji na Uwekezaji cha Bodi ya Malipo ya Uzeeni ya Kanisa la Uingereza (mwakiishi wa PRI) alisema: "Kwa miongo sasa watu wametoa wito wa kuwepo kwa viwango vya kimataifa vinavyowezesha matendo mazuri. Ni jambo la kusikitisha kuwa ni baada ya janga la Brumadinho ndiposa haya yakawezekana. Lakini, ubia wa kipekee umejitokeza ili kukabiliana na changamoto za kimfumo zinazoikumba sekta ta uchimbaji wa migodi na sasa tumejitolea kufanikisha haya katika ngazi zote za utendakazi. Kwa mara ya kwanza tuna viwango vya kimataifa vinavyofuka mipaka ya matendo mazuri na kuunda viwango kwa mapana na marefu vitakabyowezesha kampuni kuwajibika kuviteleleza.  Ninatarajia kufanya kazi na wahusika wote ili kubuni taasisi inayojitegemea itakayoweza viwango hivi kutekelezwa.

John Howchin, Katibu Mkuu, Baraza a Maadili la Uswizi Malipo ya Uzeeni ya Kitaifa (mwakilishi wa PRI) alisema: "Mnamo Januari mwaka wa 2019 tulitoa wito wa kuwepo na viwango vipya katika sekta iliyo na njia nzuri za kukabiliana na uwezekano wa kufeli kwa viwanda vya madini, na tumehakikishiwa na wataalamu wa jopo la kujitegemea la Global Tailings Review kuwa iwapo viwango hivi vingekuwepo, janga la Brumadinho halingetokea. Tunatarajia kuwa kampuni zote za uchimbaji wa mikodi zitafuata mfumo huu, na wawekezaji wazuri wanaolenga kukabiliana na uwezekano wa kufeli kwa kampuni za madini sasa wana fursa wa kuwezesha utekelezaji, kwa kutumia Viwango vilivyowkwa na mikakaati yao binafsi."

Tom Butler, CEO wa ICMM, alisema: "ICMM na wanachama wake - wanaowakilisha takribani theluthi moja ya sekta hiyo duniani - wamejitolea kwa dhati kuhakikisha usimamizi wa viwanda vya madini unafanywa kwa njia salama. Baraza la ICMM linakaribisha Viwango vya Kimataifa vya Usimamizi wa Sekta ya Uchimbaji wa Madini kama hatua muhimu ya kufikia malengo haya. Kupitia utekelezaji mzuri wa Viwango hivi, wanachama wa ICMM watakuwa mstari mbele kwa kampuni zote za uchimbaji wa migodi kushirikiana kufanya vituo vyote vya uchimbaji wa madini kuwa salama.

"Viwango hivyo vitaongezwa katika uwajibikaji wa wanachama wa ICMM, ikiwa ni pamoja na kutathminiwa na kuidhinishwa na watu wasiohusika moja kwa moja. Kwa sasa, bado tunabuni mwongozo wa kuviunga mkono. Wanachama wamejitolea kuhakikisha kuwa viwanda vilivyo na 'Uwezekano mkubwa' au 'Hatarini zaidi' vitafuata maagizo yote ya viwango hivyo katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia leo, na viwanda vingine vyote vitafanya hivyo ndani ya kipindi cha miaka tano." 

Viwango hivyo vinashughulikia mada sita kuu: jamii zinazoathiriwa; kituo cha maarifa; michoro, ujenzi, utendakazi na ufuatiliaji wa vituo vya uchimbaji wa madini, usimamiaji, ushughulikiaji wa dharura wa mikasa inapotokea na hatua za kudumu  itakazochukuliwa; na kuwezesha umma kupata taarifa kwa njia rahisi. Mada hizi zinajumuisha kanuni 15 na mambo 77 yanayoweza kutathminiwa ya kufuatwa na watendakazi.

Kuzinduliwa kwa Viwango hivyo siku ya leo kunaungwa mkono na makala mengineyo mawili, yalichapishwa na mwenyekiti wa GTR kivyake: mkusanyiko wa makala ya kina yanayoangazia njia mbalimbali za uatendakazi na usimamizi wa masuala kuhusiana na utengenezaji wa madini, na ripoti ya maoni ya umma baada ya mashauriano.

GTR inasimamiwa na Dkt Oberle akisaidiwa na jopo la wataalamu kutoka sekta mbalimbali na mchango kutoka kwa Kikosi cha Ushauri cha wadau kutoka sekta mbalimbali. Kulikuwa na majadiliano ya kina na jamii zilizoathiriwa, wawakilishi wa serikali, wawekezaji, mashirika ya kimataifa na sekta ya uchimbaji migodi na kupata maarifa kutoka njia nzuri zilizopo na utafiti wa vituo vilivyofeli vya uchimbaji wa madini.

 

MAKALA KWA WAHARIRI

Viwango vya Kimataifa vya Usimamizi wa Sekta ya Uchimbaji Madini vinapatikanahapa kwa Kiingereza, Kireno, Kirusi, Kifaransa, Kihispania, Kichina na Kijapani.

Tembelea tovuti ya GTR kwa tarifa zaidi kuhusu usimamizi, mashauriano ya kimataifa na umma rasimu ya Viwango na utangulizi kuhusu uchimbaji wa madini.

Taarifa zinazojumuisha picha kuhusu Viwango hivyo zinapatikanahapa.

Kuhusu ICMM

Baraza la Kimataifa la Uchimbaji wa Mikodi na Madini (ICMM) ni shirika a kimataifa lililojitolea kuhakikisha kuna usalama, usawa na uchimbaji wa migodi na madini kwa njia endelevu. Linaleta pamoja kampuni 27 za uchimbaji migodi na madini na zaidi  ya makundi na kanda 35 zinazotumia bidhaa hizo, inaimarisha utendakazi wa mazingira na wa jamii na kufanya kazi kama chanzo cha mabadiliko na kuimairisha manufaa ya uchimbaji wa migodi kwa jamii. Kila kampuni mwanachama wa ICMM hufuata Kanuni za Uchimbaji Migodi  zinazojumuisha kwa kina vipengele vya mazingira, vya jamii na usimamizi, uidhinishaji na wengi wa eneo la kiwanda na matarajio ya utendakazi na ahadi inayoaminika ya ripoti za uendelevu wa mradi.

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa

Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) ni mhamasishaji mkubwa wa masuala ya mazingira anayeweka ajenda ya kimataifa ya mazingira. Huwezesha Umoja wa Mataifa kutekeleza vipengele vya mazingira kwenye maendeleo endelevu, na kuhamasisha ulimwengu kuhusu maswala ya mazingira. UNEP hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.
 

Kuhusu PRI

Kanuni za Uwekezaji Mwafaka (PRI) ni mhamasishaji mkuu wa kimataifa kuhusu uwajibikaji wakati wa uwekezaji. Kufanya kazi ili kuelewa athari za uwekezaji kwa kuzingatia ESG na kuwezesha mtandao wake wa kimataifa wa wawekezaji kutekeleza yanayohitajika wakati wa uwekezaji na kuamua mmiliki. PRI hufanya kazi kuweka maslahi ya kudumu ya wanachama wake, ya masoko na uchumi wa eneo wanapopatikana, na hatimaye, ya mazingira na ya jamii nzima kwa jumla. PRI inawakilishwa katika mchakato huu na John Howchin kutoka Baraza a Maadili la Uswizi na Adam Matthews wa Bodi ya Malipo ya Uzeeni ya Kanisa la Uingereza.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na:

Antonia Mihaylova, Msimamizi wa Mradi, Global Tailings Review

Marie Daher-Corthay, Afisa wa Mawasiliano, UNEP, +973 3695 5988

Rojin Kiadeh, Mtaalamu wa Mawasiliano, Kanuni za Uwekezaji Mwafaka

Kira Scharwey, Afisa Mkuu wa Mawasiliano, Baraza la Kimataifa la Uchimbaji wa Mikodi na Madini +44 (0) 7483 092315