© UNEP/Roan Paul
07 Dec 2021 Toleo la habari Uchunguzi wa mazingira

Waleta mabadiliko watajwa kuwa Mabingwa wa Dunia wa UN wa mwaka wa 2021

© UNEP/Roan Paul
  • Tuzo la Umoja wa Mataifa la ngazi ya juu zaidi mwaka huu linamtuza waziri mkuu, mwanasayansi, wanawake wa kiasili, na mjasiriamali kwa kusababisha mabadiliko chanya kwa mazingira.
  • Mabingwa hawa wa Dunia huhamasisha, kutetea, kuhamasisha na kuchukua hatua ili kukabiliana na changamoto kuu za mazingira za wakati wetu, ikiwa ni pamoja na kutunza na kuboresha mifumo ya ekolojia.
  • Tuzo la mwaka huu linatolewa kwa washindi katika vitengo vya Mafanikio ya Kudumu,  Motisha na Kuchukua hatua, Uongozi Unaozingatia Sera, Maono ya Ujasiriamali na Sayansi na Ubunifu.

Washindi wa Tuzo la Mabingwa wa Dunia wa mwaka wa 2020 ni:

  • Waziri Mkuu Mia Mottley wa Barbados, anayetuzwa katika kitengo cha Uongozi Unaozingatia Sera kwa juhudi zake za kuhakikisha kuna dunia endelevu kwenye nchi za kipato cha chini. Mara kwa mara yeye huhamasisha kuhusu hatari inayokumba Mataifa ya Visiwa Yanayoendelea kutokana na mabadiliko ya tabianchi. Waziri Mkuu huongoza juhudi za kushughulikia mazingira katika eneo lote la Amerika Kusini na Karibean - yeye ni wa kwanza kukubali kuhusu Mikakati ya Utekelezaji wa Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo wa Ekolojia.. Chini ya uongozi wake, Barbados imeweka malengo kabambe ya nishati jadidifu, imeahidi kuwa na sekta ya umeme na uchukuzi isiyo na mafuta ya visukuku kufikia mwaka wa 2030. Wakati uo huo, Barbados inatekeleza miradi mingi ya uhifadhi na uboreshaji wa mifumo ya ekolojia, kuanzia kwa misitu, kupitia mijini, hadi ukanda wa pwani na bahari.  Ni mwenyekiti mwenza wa One Health Global Leaders' Group on Antimicrobial Resistance.
  • The Sea Women of Melanesia (Papua na Visiwa vya Solomoni), wanaotuzwa katika kitengo cha Uongozi Unaozingatia Sera, hutoa mafunzo kwa wanawake kutoka eneo hilo kufuatilia na kutathmini athari za uchujukaji wa matumbawe kwenye baadhi ya miamba ya matumbawe iliyo hatarini kuangamia kwa kutumia sayansi na teknolojia ya baharini.
  • Dkt. Gladys Kalema-Zikusoka (Uganda), anayetuzwa katika kitengo cha Sayansi na Ubunifu, alikuwa daktari wa mifugo wa  kwanza kabisa  wa Mamlaka ya Wanyamapori nchini Uganda, na ni mamlaka inayotambulika duniani inayoshughulikia wanyama wa familia ya nyani na magonjwa kutoka kwa wanyama. Akiwa Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi wa Conservation Through Public Health (CTPH), anasimamia utekelezaji wa programu tatu zilizounganishwa kimkakati kwa kutumia mbinu ya ‘Afya Moja’.
  • Maria Kolesnikova (Jamhuri ya Kyrgyz), aliyetuzwa katika kitengo cha Maono ya Ujasiriamali, ni mwanaharakati wa mazingira, mtetezi wa vijana na msimamizi wa MoveGreen, shirika linalofanya kazi kufuatilia na kuboresha hewa katika eneo la Asia ya kati. Chini ya Kolesnikova, MoveGreen ilitengeneza apu ijulikanayo kama AQ.kg, ambayo hukusanya data kila baada ya saa moja hadi tatu kutoka majiji makubwa zaidi ya Kyrgyz, Bishkek na Osh, kuhusu kiwango cha vichafuzi hewani, ikiwa ni pamoja na PM 2.5, PM 10 na dioksidi ya nitrojeni.

Kwa kuhamasisha kuhusu kazi muhimu inayofanywa na wanaharakati wa mazingira, tuzo la Mabingwa wa Dunia linalotolewa kutoa motisha kwa watu zaidi kukabiliana na changamoto tatu duniani- mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa mazingira, wa bayoanuai na uchafuzi, kemikali na taka.

Matuzo ya mwaka huu yanaangaziaMuongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha ya Mfumo wa Ekolojia, ambao unaendelea hadi 2030, unaingiliana na makataa ya kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu. Kwa kusitisha na kukabiliana na uharibifu wa mifumo ya ekolojia ya nchi kavu na majini, tunaweza kuzuia uharibifu wa viumbe milioni moja vilivyo hatarini kutoweka. Wanasayansi wanasema kuboresha asilimia 15 tu ya mifumo ya ekolojia katika maeneo yanayohitaji kushughulikiwa kwa dharura na kwa hivyo kuboresha makazi kunaweza kupunguza kuangamia kwa asilimia 60. 

Hakujawa na hitaji la dharura zaidi la kuboresha mifumo ya ekolojia iliyoharibiwa kuliko sasa.  Mifumo ya ekolojia inawezesha maisha ya viumbe wote Duniani.  Mifumo yetu ya ekolojia ikiwa dhabiti, sayari yetu itakuwa dhabiti na watu watakuwa na afya njema. Uboreshaji wa Mifumo ya Ekolojia utafaulu tu iwapo kila mtu atajiunga na vuguvugu la #GenerationRestoration ili kuzuia, kukomesha na kukabilina na uharibifu wa mifumo ekolojia kote duniani.

 

MAKALA KWA WAHARIRI

Kuhusu  Tuzo la UNEP la Mabingwa wa Dunia
Tuzo la Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa la Mabingwa wa Dunia hutuza watu binafsi, makundi na mashirika ambayo huchukua hatua za kusababisha mabadiliko chanya kwa mazingira. Tuzo linalotolewa mara moja kwa mwaka la Mabingwa wa Dunia ni tuzo la umoja wa mataifa la ngazi ya juu linalotolewa kwa heshima ya mazingira.  Hutuzwa kwa viongozi wa kipekee kutoka kwa serikali, mashirika ya uraia na sekta binafsi.

Kuhusu Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia
Baraza la Umoja wa Mataifa lilitangaza kuanzia mwaka wa 2021 hadi mwaka wa 2030 kuwa Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia. Muongo unaongozwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) la Umoja wa Mataifa na msaada kutoka kwa wabia ulibuniwa kuzuia, kukomesha na kukabiliana na uharibifu wa mifumo ya ekolojia kote ulimwenguni. Unalenga kuboresha mabililioni ya hekta za aridhi ya nchi kavu pamoja na mifumo ya ekolojia ya majini. Mwito kwa jamii ya kimatifa, the Muongo wa UN huungwa mkono na wanasiasa, utafiti wa kisayansi, na ufadhili ili kuimarisha uboreshaji.

UNEP@50: Ni wakati wa kutafakari kuhusu yaliyopita na kutazamia yajayo
Kongamano la Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira ya Binadamu mjini Stockholm, Uswidi katika mwaka wa 1972, ulikuwa mkutano wa kwanza wa Umoja wa Mataifa kutumia neno "mazingira" kwenye anwani yake kwa mara ya kwanza. Kuanzishwa kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) ni mojawapo wa matokeo makuu ya kongamano hili lilianzisha mambo mengi. UNEP ilianzishwa kuwa kitengo cha kushughulikia mazingira cha Umoja wa mataifa kote ulimwenguni. Shughuli zitakazoendelea katika mwaka wa 2022 zitaangazia hatua zilizopigwa na yatakayojiri katika miongo ijayo.

Kuhusu Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP)
UNEP ni mhamasishaji mkuu wa masuala ya mazingira duniani.  Hutoa uongozi na kuhimiza ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kupitia kwa kuvutia, kuelimisha na kuwezesha mataifa na watu kuimarisha maisha yao bila kuhatarisha yale ya vizazi vijavyo.  

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:
Moses Osani,, Afisa wa Mawasiliano, UNEP