Photo credit: Tracey Jennings/Ocean Image Bank
23 Jul 2021 Tukio Kutumia mazingira kushughulikia tabianchi

Mambo sita unayoweza kufanya kurejesha mikoko

Usidanganyike na muonekano wa kawaida: mikoko ni muhimu kukabiliana na changamoto sugu tunazokumbana nazo duniani kwa sasa. Hutunza ardhi na bahari, huteka kaboni, huchangia utoshelezaji wa uchumi na wa chakula, na ni makaazi kwa spishi adimu zaidi zinazopendeza.

Ila mikoko inadidimia katika kiwango cha kusikitisha. Kwenye sehemu fulani za eneo la Magharibi mwa Bahari Hindi – mojawapo ya maeneo mawili muhimu zaidi ya mikoko ulimwenguni, ikijumuisha Asia ya Kusini – zaidi ya asilimia 80 ya mikoko tayari imeangamia.

Muongo wa Umoja wa Mataifa (UN) wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia ni vuguvugu la kimataifa linalotoa wito wa kubadilisha tunavyoingiliana na mazingira – kuacha kuyaharibu na kuyaboresha. Hapa kuna mambo sita unayoweza kufanya kurejesha mikoko sasa.

1. Fahamu umuhimu wa mikoko.

Mangroves are a nature-based solution to help prevent floods and erosion.
Picha kutoka kwa: Matt Curnock/Ocean Image Bank

Tukiwa na mifumo dhabiti ya ekolojia tunaweza kuboresha maisha ya watu, kukabiliana mabadiliko ya tabianchi na kusitisha kuangamia kwa bayoanuai.

Utafiti wa UNEP unaonyesha kwamba mifumo ya ekolojia ya mikoko ina manufaa kwa uchumi wa kimataifa na wa ndani ya nchi, kwa kusaidia sehemu za uvuvi, kutoa vyanzo vingine vya chakula na kutunza ukanda wa pwani. Hakika, kila hekta ya msitu wa mikoko inakadiriwa kuwakilisha dola za Marekani kati ya elfu 33 na 57,000 kwa mwaka.  

Pia ni walinzi wakuu - kwa kukinga ardhi na jamii za pwani dhidi ya dhoruba, tsunami, kuongezeka kwa viwango vya usawa wa bahari na mmomomyoko. Huku ulimwengu ukiwa hatarini kushuhudia ongezeko la joto la zaidi ya nyuzijoto katika karne hii, mikoko pia ni chombo muhimu cha kukabiliana na hali hii. Huteka kaboni kutoka kwa angazaidi ya mara tano  kuliko misitu kwenye maeneo ya ardhi, na kutunza mikoko ni afueni mara 1000, kwa kilomita, kuliko kujenga ukuta wa kuzuia bahari.

Jifahamishe zaidi kuhusu mifumo ya ekolojia ya mikoko kupitia video fupi; na majukuku yake ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kupitia katuni.

2. Fahamu chanzo cha uharibifu wake.

Pollution starves mangroves of oxygen
Picha kutoka kwa: Shaun Wolfe/Ocean Image Bank

 

Makaazi kwa asilimia arobaini ya idadi ya watu duniani, maeneo ya pwani ni miongoni mwa maeneo yenye wakaazi wengi Duniani. Maendeleo yanayojiri kwenye ukanda wa pwani - kukata misitu ya mikoko ili kujenga, na kufuga samaki na kamba wadogo - nichanzo kikuu cha uharibifu wa mikoko. Ulimwenguni kote, hali hii imesababisha uangamiaji wa asilimia 20 ya mifumo ya ekolojia ya mikoko. 

Uchafuzi pia una mchango wake. Kwa sababu hutunza pwani na bahari, mikoko ni "mtego wa plastiki" kikamilifu. Mifuko ya plastiki na takataka hufunika mizizi na tabaka za mashapo, inaweza kuzuia mikoko kupata oksijeni; na inaweza kudhuru wanyama wa baharini.

3. Fanya maamuzi endelevu

A fish underwater.
Picha kutoka kwa: Tiy Saputro/ CIFOR

Maamuzi tunayofanya ni njia muhimu ya kuonyesha tunachothamini na huathiri mahitaji na matumizi. Uliza maswali kuhusu chakula unachotumia; chagua vyakula ambavyo vimepatikana kwa njia endelevu; koma kutumia plastiki inayotumika mara moja na punguza matumizi yake kwa ujumla.   

Jifahamishe zaidi kuhusu unachoweza kufanya kupitia Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) kampeni ya Bahari Safi, na pitia mifano ya maamuzi mwafaka ya uboreshaji kwenye Mwongozo wa uboreshaji wa Mifumo ya Ekolojia

4. Jifahamishe kuhusu uboreshaji unavyofanya kazi. 

People working to restore mangroves.
Picha kutoka kwa: Lorenzo Mittiga/Ocean Image Bank

Kabla ya kupanda mikoko tena, ni muhimu kuelewa chanzo cha uharibifu wa misitu au kutoweka kwake. Kama hali ya uchafuzi wa mazingira, ukataji kupita kiasi au sababu nyinginezo zinazoweza kuzuilika, mikoko inaweza kurudishwa kwa njia za kawaida.

Wakati kurudishwa kwake kunahitaji uingiliaji wa mwanadamu, ni vyema kufuata hatua muhimu, kama vile kushirikisha wanajamii, kuchagua miche ya kiasili na kuanzisha vitalu kitakavyotumika. Kujifahamisha zaidi, pitia Mwongozo wa Uboreshaji wa Mifumo ya Ekolojia , unaolezea hatua baada ya hatua.

5. Kuwa mwahamasishaji na mwanaharakati.

Mangroves
Picha kutoka kwa: Matt Curnock/Ocean Image Bank

Mtu yeyote, popote ulipo, unawezaanza kuchukua hatua leo. Jadili umuhimu wa mikoko na marafiki wako, familia, wenzako kazini na mitandaoni. Shiriki jumbe, picha na mawazo yanayokuchombea.

Iwapo hufahamu pa kuanzia, shawishiwa na wanachofanya wenzako. Nchini Kenya na Madagascar, jamii zimetambua mchango wa mikoko katika maisha yao na zinashiriki kikamilifu katika ufuatiliaji wa kaboni, upandaji miti na uhamasishaji ili kuzuia matumizi mabaya na kuhakikishia vizazi vijavyo kipato.

Ili kupata mawazo kuhusu hatua unazoweza kuchukua, cheza mchezo huu; kisha elekea kwenye Muongo wa UN wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia Kituo cha Utekelezaji kufahamu wanayofanya wengine kutekeleza kazi hii.

6. Pasa sauti yako.

Mangroves
Picha kutoka kwa: David Gross/Ocean Image Bank

Licha ya ukubwa wa changamoto, kuna suluhisho; na baadhi ya serikali tayari zinachukua hatua. Cuba, Haiti, Puerto Rico na Jamhuri ya Dominika wametoa kipaumbele kwa urejeshwaji wa mikoko kupitia mradi wa Caribbean Biological Corridor; na huko Cuba, misitu ya mikoko bado inapatikana kwa asilimia 70 ya maeneo ya pwaniPakistan imejitolea kupanda miti bilioni 10 ifikapo mwaka 2023 katika mradi ulioongozwa na Waziri Mkuu Imran Khan na kuungwa mkono na UNEP, na mamilioni - kama sio mabilioni - ya miti hii itakuwa mikoko. Ahadi za upandaji tena wa miti kwa kuzingatia nchi zinaweza patikana hapa.

Je, serikali yako inafanya nini kupanda tena mikoko - nchini mwako au nje ya nchi? Pasa sauti yako ili hatua madhubuti zichukuliwe!

Kwa habari zaidi kuhusu upandaji tena wa mikoko, wasiliana na Gabriel Grimsditch, Afisa wa Usimamizi wa Programu katika Kitengo cha UNEP cha Mifumo ya Ekolojia ya Majini na Pwani: Gabriel.Grimsditch@un.org

 

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limetangaza mwaka wa 2021 hadi wa 2030 kama Muongo wa UN wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia. Muongo unaongozwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, Muongo wa UN uliobuniwa ili kuzuia, kukomesha na kukabiliana na uharibifu wa mifumo ya ekolojia kote ulimwenguni.  Muongo wa Umoja wa Mataifa uajumuisha msaada kutoka kwa wanasiasa , tafiti za kisayansi na wafadhili ili kuimarisha uboreshaji kwa lengo la kufufua mamilioni ya hekta ya mifumo ya ekolojia ya nchi kavu na majini. Tembelawww.decadeonrestoration.org tkujifahamisha zaidi.