Shutterstock /Jane Turpie
30 Jun 2021 Tukio Nature Action

Nchini Afrika Kusini, kukabilianna na uharibifu wa ardhi kunaweza zalishia uchumi manufaa: utafiti mpya

Shutterstock /Jane Turpie

Utafiti uliozinduliwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na kutolewa wiki iliyopita unaonyesha manufaa ya kiuchumi kwa kufufua chanzo kikuu cha mito katika mkoa wa Kwa Zulu-Natal nchini Afrika Kusini. 

Ripoti hiyo iliangazia bonde la Mto Thukela, ambapo kilimo, uchungaji wa ng'ombe na kuenea kwa mimea vamizi ya kigeni vimeharibu savana dhaifu na ukanda wa mbuga. Hali hiyo imeathiri uwezo wa ardhi kukimu mahitaji na kudumisha huduma muhimu za mifumo ya ekolojia, kama vile usambazaji wa maji na utegaji wa kaboni.

Utafiti mpya, Makadirio ya gharama na manufaa ya kushughulikia uharibifu wa ardhi kwenye chanzo cha mto Thukela, KwaZulu-Natal, Afrika Kusini, ilionyesha kuwa manufaa ya kuboresha bonde la Thukela kutakuwa na manufaa mengi kuliko gharama. Ili kufikia uamuzi huo, watafiti walitumia picha za setilaiti na uwajibikiaji wa mifumo ya ekolojia kukadiria maeneo yanaotoa huduma za mifumo ya ekolojia ambayo yatahitaji mno uboreshaji.

"Nisharti tuhakikishe kuwa mazingira yanazingatiwa wakati wa kufanya maamuzi wa kiuchumi na kifedha," anasema William Speller, mtaalam wa ekolojia na bayoanuai wa UNEP. “Hii haimanishi kuwekea bei kila nyuki na kila mti. Ni kuelewa kwamba mifumo dhabiti ya ekolojia ni muhimu kwa wanadamu kuliko wakati inapoharibiwa.”

Ripoti hii mpya inatolewa majuma mawili baada ya uzinduzi wa Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia, mwamko mpya wa kimataifa wa kufufua mazingira asili duniani. Shughuli za binadamu zimeharibu mno takribani asilimia 75 ya nchi kavu na asilimia 66 ya mazingira ya baharini, na kufanya mifumo mingi ya ekolojia kuwa karibu kuporomoka.

Kuwajibikia mifumo ya ekolojia

Kuwajibikia mifumo ya ekolojia kunawezasaidia kusitisha na kukabiliana na uharibifu, wasema wataalamu. Kukadiria thamani ya huduma zinazotolewa na mazingira kwa binadamu, kunawezesha watungasera kutumia vipimo vya uchumi mbali na vya jadi, kama vile pato la taifa, na kupata uelewa bora kuhusu athari za maendeleo ya kiuchumi kwa mazingira.

Kuhusu ripoti ya Mto Thukela River, watafiti waliunda akaunti ya kufanyia majaribio ya huduma za mifumi ya ekolojia kwa kuzingatia Uwajibikiaji wa Mifumo ya Uchumi wa Mazingira- Uwajibikiaji wa Mifumo ya Ekolojia (SEEA EA), viwango vya kimataifa vya kuwajibikia mifumo ya ekolojia vilianza kufanya kazi mwezi wa Machi mwaka huu.

Watafiti waligundua kuwa kurudisha nyasi kwenye maeneo makubwa ya nyanda, hasa kwa kuondoa mimea geni vamizi, kutekeleza usimamizi endelevu wa ardhi na kushughulikia mmomonyoko wa udongo kwa kupanda miti tena, kutaboresha uwezo wa bonde wa kuhifadhi kaboni, kusababisha hifadhi kubwa ya vyakula vya porini na dawa, kukuza nyanda za uzalishaji zaidi za malisho kwa wafugaji wa mifugo, na kuimarisha usambazaji wa maji. (Mimea vamizi, kama mikalatusi, ina kiu.)

"Utafiti huu unaonyesha kuwa kuwekeza katika hatua za kupunguza, kukomesha na kukabiliana na athari halisi za usimamizi mbaya wa ardhi uliofanyika hapo awali kunaweza kuwa na manufaa makubwa na kwamba kushughulikia uharibifu wa ardhi kunaweza kukadiriwa kiuchumi," anasema Jane Turpie wa Washauri wa Mazingira wa Anchor (Anchor Environmental Consultants), mwandishi mkuu wa ripoti hiyo.

Utafiti huo unaangazia jinsi uboreshaji wa mazingira unavyoweza kusaidia kufikia malengo ya maendeleo ya kitaifa nchini Afrika Kusini, kama vile utoshelezaji wa maji na maendeleo ya vijijini, anasema Mandy Driver wa Taasisi ya Kitaifa ya Bayoanuai ya Afrika Kusini. "Inaonyesha kuwa kuwekeza katika miundomsingi ya ekolojia ni muhimu kama vile kuwekeza kwenye aina nyinginezo za miundomsingi ya kijamii na kiuchumi, kama vile mabwawa na mitandao ya uchukuzi."

Hii haimanishi kuweka bei kwa kila nyuki na kila mti. Ni kuelewa kwamba mifumo dhabiti ya ekolojia ni muhimu kwa wanadamu kuliko wakati inapoharibiwa.

William Speller, UNEP

Ripoti ya Thukela ni sehemu ya mradi wa Uwajibikiaji wa Mtaji Asilia na Ukadiriaji wa Huduma za Mifumo ya Ekolojia ambao Afrika Kusini ilikuwa mojawapo ya washiriki. Afrika Kusini imetia sahihi Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Kuenea kwa Majangwa na inalenga kufikia "kutokuwapo kwa uharibifu wa ardhi" kuifikia mwaka wa 2030.

Kiruben Naicker wa Idara ya Misitu, Uvuvi na Mazingira ya Afrika Kusini alisema kuwa ripoti hiyo itasaidia kuelekeza upya uwekezaji "unapohitajika zaidi na inayosaidia harakati ya ukusanyaji wa rasilimali".

Utafiti wa Thukela ni sehemu ya juhudi pana za UNEP za kuhakikisha mazingira yanajumuishwa kwenye maamuzi ya kiuchumi na kifedha. Speller anasema mbinu zinazotumiwa katika bonde la Mto Thukela zinaweza kutumika kwa mifumo ya mazingira iliyoharibika kote ulimwenguni. “Mfumo huo mpya unaweza kubadilisha mambo wakati wa kufanya maamuzi. Kwa kuonyesha mchango wa mazingira, sasa tuna chombo kinachoturuhusu kupima vizuri na kuthamini mazingira. Inaweza kutusaidia kuleta mabadiliko ya haraka na ya kudumu kuelekea uendelevu kwa watu na mazingira."

 

Unajumuisha nchi za Brazil, China, India, Meksiko na Afrika kusini mradi wa Uwajibikiaji wa Mtaji Asilia na Ukadiriaji wa Huduma za Mifumo ya Ekolojia, utakaondeshwa hadi mwishoni mwa mwaka wa 2021, unalenga kuimarisha maarifa ya ajenda ya uwajibikiaji wa mazingira na uchumi. Mradi unaofadhiliwa na Muungano wa Ulaya, na kutekelezwa na Idara ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa, UNEP, na Sekretarieti ya Mkataba wa Uanuai wa Kibaolojia, wabia wa mradi huu nchini Afrika Kusini ni pamoja na Takwimu Afrika Kusini, Taasisi ya Kitaifa ya Bayoanuai ya Afrika Kusini (Statistics South Africa), na Idara ya Misitu, Uvuvi na Mazingira ya Afrika Kusini.

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa limetangaza miaka ya 2021 hadi 2030 kuwa Muongo wa UN wa uboreshaji wa Mifumo ya Ekolojia. Ukiongozwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa na Shirika la Chakula na Kilimo, Muongo wa UN umeundwa kuzuia, kukomesha na kukabiliana na uharibifu wa mifumo ya ekolojia kote ulimwenguni. Wito huu wa kimataifa wa kuchukua hatua ulizinduliwa tarehe 5 Juni, Siku ya Mazingira Duniani. Utajumuisha msaada wa kisiasa, utafiti wa kisayansi na mchango wa kifedha ili kuimarisha uboreshaji kwa lengo la kufufua mamilioni ya hekta za mazingira ya ardhini na majini. Pitia kazi ya UNEP kuhusu kuhifadhi kwa mifumo ya ekolojia, ikijumuisha misitukanda za pwanimboji na matumbawe. Fjifahamishe zaidi Muongo wa UN wa uboreshaji hapa

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na Will Speller: william.speller@un.org