Picha na Unsplash/Lenstravelier
20 Jul 2022 Video Kushughulikia Mazingira

Jinsi tunavyoweza kutunza miji dhidi ya mawimbi ya joto

Sayari inapoendelea kukakabiliwa na joto, hitaji la viyoyozi duniani litaongezeka, na kuzalisha gesi zaidi ya ukaa hali itakayojirudia vibaya. Lakini kuleta miti na maeneo ya kijani mijini mwetu ni suluhisho lililo na manufaa mengi. Miti haitoi tu kivuli ambacho hupunguza gharama za viyoyozi, lakini pia hupunguka joto katika angani kwa kutoa maji kupitia kwenye matawi yake - sawa na wanadamu wanapotoa jasho kupungaza joto. Kwa hakika, wataalamu wanadai kwamba miti huchangia hadi dola milioni 500 kwa chumi za ‘miji mikubwa’ kutokana na manufaa yanayotokana na kupoesha na kuchuja hewa chafu.