Unsplash / Jason Ortego
17 Mar 2021 Video Kutumia mazingira kushughulikia tabianchi

Kulinda misitu ya Mlima Kenya

Unsplash / Jason Ortego

Askaripori wa Mt. Kenya Trust hufanya kazi bila kuchoka kulinda misitu na wanyamapori wa eneo hilo dhidi ya vitendo haramu kama vile ukataji wa miti na uwindaji haramu. Dhamira yao ni kuhifadhi ekolojia hii ya kipekee na kuelimisha jamii za wenyeji kuhusu manufaa ya kuhifadhi misitu ya Mlima Kenya.

Filamu hii ilichukuliwa na Joan Poggio kutumiwa kwa Kampeni ya Wild for Life ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, kama sehemu ya mfulilizo wa video zinazojumuisha visa binafsi vya walio mstari mbele kuhamasisha kuhusu wanyamapori.

Fanya safari ya kina kwenye misitu ili ugundue jinsi mifumo hii ya ekolojia inayothaminiwa inavyonufaisha wanadamu na wanyamapori kila siku.