Photo by UNEP
19 Nov 2020 Video Kushughulikia Mazingira

Kuunda fueli isiyochafua mazingira kutoka kwa taka nchini Kenya

Photo by UNEP

Tarehe 19 Novemba ni Siku ya Choo Duniani. . Kaulimbiu ya mwaka wa 2020 ni usafi endelevu na mabadiliko ya tabianchi.

Siku ya Choo Duniani inasherehekea kuwepo kwa vyoo na inahamasisha kuhusu watu bilioni 4.2 wanaoishi bila kupata huduma za usafi kwa njia salama. Inahusu kuchukua hatua kukabiliana na shida ya usafi ulimwenguni na kufikia Lengo la Maendeo Endelevu la 6 : maji na usafi kwa wote ifikapo mwaka wa 2030.

Kwenye mwambao wa Ziwa Naivasha nchini Kenya, kampuni ya uvumbuzi inafanya kazi kusuluhisha kwa wakati mmoja maswala ya ukataji miti na usafi duni. Vipi? Kwa kutumia kinyesi kutengeneza makaa endelevu yasiyochafua mazingira. Kampuni hiyo, Sanivation, hutumia mchakato unaotumia jua kugeuza taka kuwa nishati, kielelezo kizuri kwa biashara na kwa mazingira.