Kushiriki kwa Mashirika ya Uraia

Kushiriki kwa Mashirika ya Uraia

Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) linatambua umuhimu wa kushirikisha Makundi Makuu mbali na Wadau wengine kama washirika na kujivunia mielekeo wanayoleta, tafiti muhimu na uhamasishaji wanaofanya na wajibu wao wa mda mrefu, ulio mpana wa kuunga mkono dhamira ya UNEP.

Uamuzi unaofanywa na serikali mbalimbali utatamba kote, kuimarika na kuungwa mkono na serikali iwapo maoni ya Makundi Makuu na Wadau yatazingatiwa mapema ipasavyo wakati wa michakato ya kutunga sera na kufanya mauamuzi. Makundi Makuu na Wadau pia huwa mstari mbele wakati wa utungaji sera; wao hufanya kazi kama watafiti, washauri, wanaharakati au wahamasishaji.

Soma zaidi

Kujenga Ushirikiano Mzuri Kikamilifu kati ya Makundi Makuu na Wadau(MGS) na UNEA 5.2 na UNEP  Webinar ya UNEP MGS - Kuwajengea Uwezo wa UNEA 5.2

Kuandaa Makundi Makuu na Wadau (MGS) kushiriki kikamilifu kwenye UNEA 5.2, kwa msaada wa UNEP, Jukwa la Wadau wa Mustakabali Endelevu (https://stakeholderforum.org/) liliandaa msururu wa mafundinzo kwa kanda zote sita miezi minne mwishoni mwa mwaka wa 2021.

Makala kwenye lugha za  KiarabuKifaransa, na Kihispania ya webinar hizo zilizorekodiwa yanapatikana mbali na ya Kiingereza. Makala yaliyorekodiwa ya webinar zote tano yanaweza patikana kwenye wavuti ya Jukwa la Wadau wa Mustakabali Endelevu ukrasa wa Webinar za SF.

Mawasilisho kwa lugha ya Kiingereza na Kihispania yako tayari, tafsiri ya Kifaransa itakuwa tayari hivi karibuni.

UNEP@50 na UNEP Tunayotaka

Soma zaidi

 

 

Mitazamo

Issue No. 49: Breaking Down EPR Policy and Why it Makes a Difference for Recycling System Change

In issue 49 of Perspectives, the Recycling Partnership's comprehensive analysis of worldwide EPR programs underscores the potential impact of this policy in the U.S.

See all perspectives

Rasilimali

Katika ukrasa unaofuata utapata rasilimali mbalimbali kama vile miongozo ya uchapishaji na makala ya sera ambayo UNEP (Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa) imeandalia Makundi Makuu na Wadau wa mashirika ya uraia.

Jifahamishe zaidi

Mashirika yaliyoidhinishwa

Makundi Makuu na Wadau wanaweza kushirikiana moja kwa moja na UNEP kwa kutuma maombi ya Kuidhinishwa na Baraza la Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA) la UNEP. Jifahamishe zaidi

Contact us

Kwa maelezo zaidi, wasiliana na Kitengo cha Mashirika ya Uraia:

Barua pepe: unep-civilsociety@un.org

Simu: +254 20 76 24500