Kazi yetu katika eneo la Amerika Kaskazini

Afisi ya eneo la Amerika Kaskazini ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UN Environment) ilianzishwa Washington, D.C. mwaka wa 2000. Dhima yetu ni kuendeleza kazi ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa kote ulimwenguni kwa kuhimiza kuwepo kwa ushirikiano na kujenga ubia kati ya wadau kutoka Amerika Kaskazini na jamii nzima ya kimataifa ili kushughulikia masuala yanayoathiri mazingira. 

Kupitia kwa ushirikiano na serikali za Marekani na Kanada, mashirika ya uraia, sekta ya kibinafsi, jumuia za wasomi na wanasayansi, tunanuia kukuza Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya 2030 kwa njia itakayohifadhi mazingira na kuyafanya yarejee kwa hali yake asilia, kuboresha maisha ya binadamu na hata kuwa na matumaini kuwa vizazi vijavyo vitanufaika.. 

Katika eneo la Amerika Kusini, kazi yetu ni: 

  • Kuelimisha na kushirikisha serikali za kitaifa na serikali za mtaa kutoka katika eneo hili katika kazi ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa;
  • Kuanzisha ushirikiano mpya na wabia na kukuza rasilimali za kiteknolojia, kielimu na kifedha kwa miradi ya ndani ya nchi na ya kimataifa;
  • Kushirikiana na sekta za kibnafsi ili kuongeza idadi ya taasisi kutoka eneo la Amerika Kaskazini zinazoshiriki katika taasisi za Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa- hasa kwa miradi na programu zake maalum;
  • Kuhimiza mashirika makuu ya uraia kutoka eneo la Amerika Kusini kuwa mstari wa mbele katika kutekeleza sera na shughuli za Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa;
  • Kushirikisha watumiaji wa bidhaa kushughulia changamoto kuu zinazokabili mazingira kupitia kampeni kwa umma.

 Jopo la Washauri wa Sayansi na Teknolojia (STAP) hupatikana katika Afisi ya Amerika Kaskazini ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa. STAP ni shirika linalotoa ushauri kwa Mfuko wa Mazingira Duniani na hutoa ushauri usiokuwa na upendeleo, wa kisayansi na wa kiufundi kuhusu sera, mikati ya utendakazi, programu na miradi; na lina kihifadhidata cha taasis, mitandao ya wanasayansi na wanasayansi binafsi wa kutumika kama wataalamu au kutoa ushauri inapohitajika.