26 October 2021 Ripoti

Ripoti ya Uzalishaji wa Gesi Chafu ya Mwaka wa 2021

Waandishi: UNEP, UNEP DTU Partnership
img

Mabadiliko ya tabianchi yanapozidi kuwa mabaya huku wanasayansi wakitoa onyo kuwa binadamu wanapoteza fursa ya kudhibiti ongezeko la joto duniani lisizidi nyuzijoto 1.5 zaidi ya viwango vinavyohitajika, mwaka wa 2021 haujatendea mazingira haki. 

Ripoti ya Uzalishaji wa Gesi Chafu ya Mwaka wa 2021 Joto Linazidi Kuongezeka ni toleo la 12 la msururu wa ripoti zinazotolewa mara moja kwa mwaka zinazoenyesha tofauti kati ya hali halisi ya uzalishaji wa gesi ya ukaa na makadirio kufikia mwaka wa 2030 na inavyostahili kuwa ili kukabiliana na madhara mabaya ya mabadiliko ya tabianchi. 

Yepi ni mapya kwenye hii ripoti 

Ripoti ya Uzalishaji wa Gesi Chafu ya Mwaka wa 2021 inaonyesha kuwa ahadi mpya za mazingira zikijumuishwa na mikakati mingineyoya kushughulikia mazingira inaonyesha ulimwengu unaenda kushuhudia ongezeko la joto la nyuzijoto 2.7 kufikia mwisho wa karne hii. Hiki ni kinyume cha malengo la Mkataba wa Paris kuhusu mazingira na itapelekea mabadiliko mabaya mno kwa mazingira Duniani. Ili kufaulu kudhibiti ongezeko la joto duniani lisizidi nyuzijoto 1.5 katika karne hii, kama inavyojitokeza kwenye malengo ya Mkataba wa Paris, dunia inahitaji kupunguza nusu ya uzalishaji wa gesi chafu kwa kipindi cha miaka nane ijayo.  

Zikitekelezwa kikamilifu, ahadi za kutozalisha gesi chafu zinaweza kudhibiti ongezeko la joto lisizidi nyuzijoto 2.2, kiwango karibu na nyuzijoto 2 kilicho kwenye malengo ya Mkataba wa Paris.  Hata hivyo, nyingi ya mipango ya kitaifa ya kushughulikia mazingira itaanza kushughulikiwa baada ya mwaka wa 2030.

Kupunguza uzalishaji wa methani kutoka kwa mafuta ya visukuku, taka na sekta za kilimo kunaweza kuchangia kupunguza pengo la uzalishaji wa gesi chafu na kupunguza ongezeko la joto kwa kipindi kifupi. 

 Masoko ya kaboni pia yanaweza kusaidia kupunguza uzalishaji wa gesi chafu. Lakini haya yatatokea tu iwapo sheria zitafafanuliwa wazi na zilenge upunguzaji halisi wa uzalishaji wa gesi chafu, na huku zikiungwa mkono na mipango ya kufuatilia maendeleo kwa njia ya uwazi.   

Emissions Gap Report 2021 - Publication launch

The United Nations Environment Programme (UNEP) will launch the Emissions Gap Report 2021 in a high-level online press event.

Updated climate commitments ahead of COP26 summit fall far short, but net-zero pledges provide hope

Latest UNEP Emissions Gap Report finds new and updated Nationally Determined Contributions only take 7.5% off predicted 2030 emissions, while 55% is needed to meet the 1.5°C Paris goal