04 March 2019 Ripoti

Hali ya Mazingira Duniani- GEO-6

Waandishi: UNEP
Jalada la GEO

Ripoti iliyochapishwa kwa wakati wa Kikao cha Nne cha Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa, Ripoti ya sita ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa ya Hali ya Mazingira Duniani (2019) inatoa wito kwa wafanya maamuzi kuchukua hatua za kushughulikia masuala muhimu ya mazingira haraka ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu pamoja na Malengo mengine ya Mazingira Yaliyokubalika Kimataifa, kama vile Mkataba wa Paris.

Baadhi ya jumbe muhimu kutoka kwenye ripoti hiyo

1. Ripoti ya sita ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa ya Hali ya Mazingira Duniani (GEO-6) ni ya kina zaidi kuhusu mazingira duniani tangu mwaka wa 2012.  Inaonyesha kuwa hali ya jumla ya mazingira duniani inazidi kuzorota na fursa ya kushughulikia hali hiyo inaendelea kupungua.

2. GEO-6 inaonyesha kuwa mazingira ni nguzo na msingi wa ustawi wa kiuchumi, afya ya binadamu na ustawi.  Inaangazia changamoto kuu kwa Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu: kwamba hakuna mtu anayepaswa kuachwa nyuma, na kwamba kila mtu anapaswa kuishi maisha yenye afya, mazuri kwa manufaa kamili kwa wote, kwa vizazi vilivyopo na vizazi vijavyo.

3. Mifumo isiyo endelevu ya uzalishaji na ruwaza na mienendo isiyoendelevu na ukosefu wa usawa vikijumuishwa na ongezeko la matumizi ya rasilimali kutokana na ongezeko la watu, ni tishio kwa sayari bora inayohitajika ili kuwa na maendeleo endelevu.  Mienendo hiyo inasababisha kuzorota kwa hali ya sayari kwa viwango ambavyo havijawahi kushuhudiwa, kukiwa na madhara mbaya zaidi, haswa kwa watu maskini na maeneo maskini.

4. Zaidi ya hayo, ulimwengu hauelekei kufikia vipengele vya mazingira vya Malengo ya Maendeleo Endelevu au malengo mengine ya mazingira yaliyokubaliwa duniani kufikia mwaka wa 2030; wala hauelekei kufikia uendelevu wa muda mrefu kufikia mwaka wa 2050.  Hatua za dharura na ushirikiano wa kimataifa ulioimarishwa
vinahitajika kwa dharura ili kubadili mielekeo hiyo ghasi na kurejesha ubora wa sayari na afya ya binadamu.

5. Uzalishaji wa gesi ya ukaa zamani na za sasa tayari umepelekea dunia kushuhudia kipindi kirefu cha mabadiliko ya tabianchi huku madhara anuai yakitokea kwa mazingira na kwa jamii nzima.

GEO-6: Sayari Bora, Watu wenye Afya

Ripoti ya sita ya Hali ya Mazingira Duniani, au (GEO-6) ndiyo ripoti ya kina zaidi ya mazingira duniani, inayoshughulikia mada na masuala mbalimbali, na masuluhisho yanayowezekana. Kwa sasa, ulimwengu hauelekei kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu. GEO-6 ya UNEP inatoa wito wa kutunga sera zitakazoshughulikia mifumo yote ili kuwa na maisha bora kwa watu wote.

Afya ya binadamu iko hatarini zaidi ikiwa hatua za dharura hazitachukuliwa kutunza mazingira, yaonya ripoti muhimu ya Umoja wa Mataifa

Nairobi, Kenya, Machi 13, 2019 - Tathmini ya kina na pana zaidi kuhusu hali ya mazingira iliyofanywa na UN katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ilichapishwa leo, ikionya kwamba uharibifu wa sayari ni mbaya sana hivi kwamba afya ya watu itazidi kuathiriwa iwapo hatua za dharura hazitachukuliwa.  Ripoti hiyo, iliyoandaliwa na wanasayansi 250 na wataalam kutoka zaidi ya nchi 70,…

Hadithi Inayoingiliana ya GEO-6

Ripoti ya sita ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa ya Hali ya Mazingira Duniani (GEO-6) ni tathmini ya kina zaidi kuhusu hali ya mazingira duniani. Ripoti hiyo pia inachanganua kwa kina uwezekano wa kuwa na mustakabali bora. Tumepiga hatua, ila safari bado. Ni wakati kwetu sote kuelewa mabadiliko yatakayohitajika kutunza hali ya sayari yetu.

Unaweza pia kupendezwa na nyenzo zifuatazo