27 October 2022 Ripoti

Ripoti ya Emissions Gap mwaka wa 2022

Waandishi: UNEP
Jalada la EGR 2022

Huku athari za mabadiliko ya tabianchi zinazoshuhudiwa zinapoongezeka kote duniani, ujumbe kwamba uzalishaji wa gesi chafu sharti ukome hauna utata. Ripoti ya Emissions Gap Mwaka wa 2022: Fursa inayodidimia – Changamoto za mazingira zinapaswa kushughulikiwa kwa dharura katika jamii  inabaini kwamba jamii ya kimataifa ingali mbali kabisa kufikia malengo katika Mkataba wa Paris, na inakosa mikakati ya kuaminika ya  kufikia nyuzijoto 1.5. Ni mabadiliko tu ya dharura ya mfumo mzima yanayoweza kuzuia maafa kwa mazingira. 

Mambo mapya katika ripoti ya mwaka huu 

Ripoti hii ni toleo la 13 katika mfululizo wa ripoti ya kila mwaka inayotoa muhtasari wa tofauti kati ya hali ya uzalishaji wa hewa chafu unavyotarajiwa kuwa katika mwaka wa 2030 na inavyopaswa kuwa ili kuzuia athari mbaya zaidi za mabadiliko ya tabianchi.

Ripoti inaonyesha kwamba ahadi zilizosasishwa za kitaifa tangu kutokea kwa COP26 - iliyofanyika mwaka wa 2021 mjini Glasgow, Uingereza - zinapelekea mabadiliko machache ikilinganishwa na makadirio ya mwaka wa 2030 ya uzalishaji wa hewa chafu na kwamba tungali mbali kufika lengo la Mkataba wa Paris la kudhibiti ongezeko la joto duniani lisizidi nyuzijoto 2, au ikiwezekana nyuzijoto 1.5. Utekelezaji wa sera zilizopo kwa sasa utapunguza tu ongezeko la joto hadi kati na nuzijoto 2.4 na 2.6 kufikia mwisho wa karne hii, kwa ahadi zinazotolewa kwa hiari na zile zinazotolewa kwa masharti mtawalia.  

Ripoti hiyo inabaini kuwa ni mabadiliko ya haraka ya mfumo mzima tu ndiyo yanayoweza kudhibiti uzalishaji wa hewa chafu unaohitajika kufikia mwaka wa 2030: Asilimia 45 ikilinganishwa na makadirio kwa kuzingatia sera zilizopo kwa sasa ili kuwezesha kufikia nyuzijoto 1.5 na asilimia 30 kufikia nyuzijoto2. Ripoti hii inaangazia kwa undani jinsi ya kuleta mabadiliko haya, kwa kuangazia hatua zinazohitajika katika sekta ya usambazaji wa umeme, viwanda, uchukuzi na ujenzi, na mifumo ya chakula na fedha. 

Janga la hali ya hewa linahitaji jamii kufanyiwa mabadiliko kwa dharura

Fursa inadidimia! Dunia ingali mbali kufikia malengo ya Mkataba wa Paris na kiwango cha joto duninani kinaweza kufikia nyuzijoto 2.8 kufikia mwishoni mwa karne hii. Ripoti ya Ripoti ya Emissions Gap Mwaka wa 2022 inabaini kuwa dunia lazima ipunguze uzalishaji wa hewa chafu kwa asilimia 45 ili kuepuka janga la kimataifa. Masuluhisho ya kubadilisha jamii yapo, ila wakati wa kuchukua…

Uzinduzi wa Ripoti: Ripoti ya Emissions Gap mwaka wa 2022

Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) litazindua toleo la mwaka wa 2022 la Ripoti ya Emissions Gap Mwaka wa 2022: Fursa inayodidimia – Changamoto za mazingira zinapaswa kushughulikiwa kwa dharura katika jamii  kwa vyombo vya habari mtandaoni tunapoelekea Kongamano la Umoja wa Mataifa la Mazingira la Mwaka wa 2022 (COP27).

Fufua fursa inayodidima ya kushughulikia mazingira

Sitapoteza muda wako kwa kuzungumzia athari za mabadiliko ya tabianchi. Sisi sote tunazifahamu. Sisi sote tunazishuhudia. Sisi sote tunajua kuwa zinazidi kuwa mbaya zaidi. Na bado, kama Ripoti ya UNEP ya Emissions Gap Mwaka wa 2022 inavyoonyesha, sisi bado, BADO, hatuchukui hatua za kutosha kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa.