Ripoti ya "Emissions Gap Report" ya mwaka wa 2019

26 November 2019
Authors: UN Environment Programme

Toleo la ripoti ya "Emissions Gap Report" litachapishwa tarehe 26 mwezi wa Novemba mwaka wa 2019

Dunia inapoweka juhudi ili kupunguza uzalishaji wa gesi ya ukaa na kudhibiti mabadiliko ya tabianchi, ni muhimu kufuatilia umbali uliosalia kufikia malengo ya mazingira duniani. Kwa karne moja, ripoti ya UNEP ya "Emissions Gap Report"  huangalia mwenendo wa uzalishaji wa gesi ya ukaa na kulinganisha na vile inavyohitaji kuwa, na kuanisha mbinu mwafaka za kupunguza pengo lilopo..

Ni yepi mapya katika ripoti ya mwaka huu?

Maelezo kuhusu pengo la uzalishaji wa hewa chafu

Ripoti hii itoa data iliopo kuhusu pengo lililosalia kweza kufikia nyuzijoto 1.5 zinazotarajiwa kufikiwa ifikiapo mwaka wa 2030 kwa mjibu wa Mkataba wa Paris. Inaangazia hali tofautitofauti kutoka mwaka wa 2005 wakati hapakuwepo na sera yoyote  kuhusu mazingira hadi wakati wote wa utekelezaji wa ahadi za kitaifa kwa kuzingatia Mkataba wa Paris. Kwa mara ya kwanza,  inaangalia jinsi upunguzaji mkubwa wa hewa chafu kila mwaka unahitaji kuwa tangu mwaka wa 2020 hadi mwaka wa 2030 ili kuendelea na mwenendo utakaowezesha kufikia malengo ya Mkataba wa Paris.

Jinsi ya kukabiliana na pengo la uzalishaji wa hewa chafu.

Kila mwaka, ripoti hiyo huangazia jinsi ya kupunguza pengo lililopo. Mwaka huu, ripoti inaangalia uwezekano wa kubadili nishati inayotumiwa - hasa katika sekta ya nguvu za umeme, ya usafiri na ya ujenzi-na utumiaji kikamilifu wa vifaa kama vile chuma na simiti.