Kuhusu

Kuhusu

Vijana Bingwa Duniani

 

Kupitia Vijana Bingwa Duniani – Tuzo la kifahari zaidi linalotolewa na Umoja wa Mataifa kwa vijana wanaoshughulikia mazingira– UNEP inasaka vijana wanaoleta mabadiliko kupitia mawazo na masuluhisho yao ya kipekee yanayonyesha uwezo wa mazingira kushughulikia changamoto za aina tatu duniani.

Janga la mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa bayoanuai na uharibifu wa mazingira na ongezeko la uchafuzi na viwango vya taka ni tishio kwa mifumo ya ekolojia ya kiasili na kwa jamii. Vijana wenye maono wanahitajika wanaona fursa mbali na majanga haya na kuwa na ujasiri wa kuvumbua kwa manufaa ya siku zijazo kwa kujichukulia nafasi zao katika jamii mpya isiyochafua mazingira.   

Vijana wanabebeshwa mzigo mkubwa kutokana na kuongezeka kwa ukosefu wa usawa na ukosefu wa ajira. Wanahitaji kufikia vyema mitandao na mtaji, kiti katika meza ya kufanya maamuzi kuhusu mazingira, na ushauri na mafunzo maalum.  

Katika mwaka wa 2024, vijana - watakaochaguliwa kutoka pembe zote za dunia - watajulikana kama Vijana Bingwa Duniani. Washindi hawa watapokea mtaji, mafunzo ya kina na ushauri maalum ili kufanikisha mawazo yao makubwa kuhusu mazingira. UNEP inatafuta wasanii, wanasayansi, wanauchumi, wawasilianaji na wajasiriamali vijana kutoka matabaka yote maishani ambao wana mawazo makubwa, ya ujasiri - kwa manufaa ya mazingira binadamu na kwa siku zijazo zisizo na uchafuzi. 

JIFAHAMISHE ZAIDI KUHUSU JINSI UNAVYOWEZA KUTUMA MAOMBI YA KUSHIRIKI

Image removed.
Young Champions Brochure

Explore More