Mabingwa wa Dunia ni mpango mkuu unaoshirikisha vijana wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP). Tuzo hili hutolewa kila mwaka kwa vijana wanajitolea kote ulimwenguni walio na mawazo bora ya kutunza na kuboresha mazingira.

Binadamu wanatumia sawa na 1.6 Dunia kuendeleza jinsi tunavyoishi, na mazingira hayawezi kuendelea kustahimili. Bahari inasakamwa na plastiki, mito inazidi kuchafuliwa, misitu inateketea, na udongo wa mashambani unakauka.

Kupitia Vijana Bingwa Duniani – Tuzo la kifahari zaidi linalotolewa na Umoja wa Mataifa kwa vijana wanaoshughulikia mazingira– tunasaka vijana wanaoleta mabadiliko kupitia mawazo na masuluhisho yao ya kipekee yanayonyesha uwezo wa mazingira kushughulikia changamoto za aina tatu duniani.

Tuma maombi ya kushiriki hapa

Habari na Matukio

Sisi ni kizazi ambacho kinaweza kufanya amani na mazingira.
Sisi ni Generation Restoration.