UNEP
27 Apr 2024 Tukio Kutumia mazingira kushughulikia tabianchi

Maswali: Je! Una uelewa kiasi gani kuhusu ardhi iliyoharibiwa, majangwa na ukame?

UNEP

Zaidi ya hekta bilioni 2 za ardhi zimeharibiwa, na kuathiri mabilioni ya watu na kutishia zaidi ya nusu ya pato la taifa (GDP) duniani. Tunapokaribia nusu ya Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mifumo ya Ekolojia, serikali, mashirika ya uraia na sekta ya kibinafsi wanapaswa kuchukua hatua za dharura kutunza na kuboresha mifumo ya ekolojia. Uboreshaji wa mifumo ya ekolojia huboresha maisha, hupunguza umaskini, hujengea uwezo wa kukabiliana na hali mbaya ya hewa na kupunguza kasi ya changamoto za aina tatu duniani za mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa mazingira na bayoanuai, na uchafuzi na taka.

Tunapoelekea Siku ya Mazingira Duniani tarehe 5 Juni, pima uelewa wako kuhusu majanga makubwa zaidi yanayokabili mifumo yetu ya ekolojia.

Tunapoelekea Siku ya Mazingira Duniani, pima uelewa wako kuhusu majanga makubwa zaidi yanayokabili mifumo yetu ya ekolojia.