Горы

Kuhusu UNEP@50

Mwaka wa 2022 ni wa kipekee kwa jamii ya mazingira ulimwenguni na kwa UNEP. Ni maadhimisho ya miaka hamsini tangu kutokea kwa Kongamano la Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira la Mwaka wa 1972, ambalo linajulikana sana kama mkutano wa kwanza kuhusu mazingira. Kongamano la Stockholm la Mwaka wa 1972 lilipelea kuanzishwa kwa wizara na mashirika ya mazingira kote ulimwenguni, na kuanzisha kwa makubaliano mapya duniani ya kushirikiana kutunza mazingira na kupeleakea kuanzishwa kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa  (UNEP).

Kwa kipindi cha miaka 50 UNEP imeratibu juhudi za kimataifa za kukabiliana na changamoto kuu za mazingira duniani.   Ushirikiano huu wa kimataifa umesaidia kukarabati tambiko la ozonikukomesha matuzi ya mafuta yaliyo na risasikukomesha spishi zilizo hatarini kuangamia na kadhalika. Uwezo wa UNEP wa kuitisha mikutano na kufanya utafiti wa kiwango cha juu umetoa jukwaa kwa nchi wanachama kujadiliana, kuchukua hatua dhabiti na kukuza ajenda ya kimataifa ya mazingira.

Kuadhimisha miaka hamsini tangu kuanzishwa kwa UNEP, msururu wa shughuli zitaendelea mwaka mzima chini ya kaulimbiu ya UNEP@50. Hii ni kutambua hatua muhimu zilizopigwa kuhusiana na masuala ya mazingira duniani na kushughulikia changamoto ambazo zinawezatokea.

Haya yanatoa jukwaa kwa kikao maalum cha Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA) kinachoendeshwa mjini Nairobi, Kenya na mtandaoni, tarehe 3 na 4 Machi, 2022. Hafla hii ya ngazi ya juu inayojulikana kama UNEP@50 itatengewa maadhimisho ya miaka hamsini tangu kuanzishwa kwa UNEP katika mwaka wa 1972. Kaulimbiu ya hafla ya UNEP@50 ni "Kuimarisha UNEP ili kutekeleza kipengele cha mazingira cha Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu."

Latest news and updates