Mafanikio ya Kudumu Award

Tuzo hili huchaguliwa na kutolewa na Katibu Mkuu Mtendaji wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) Hutambua juhudi zilizochukuliwa pasipo na kusita kwa naiaba ya sayari na wanaoishi ndani yake. Sifa inayoweza kuigwa kutokana na washindi hawa ni kujitolea kwao. Wao hushiriki maarifa yao kuwa tunawza kukabaliana na changamoto za aina tatu zinazokumba mazingira; mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa bayoanuai na uchafuzi iwapo tutachukua hatua mwafaka.

UNEP husimamia na kuwa mwenyeji wa matuzo ya Mabingwa wa Dunia.  Sifa ya kimataifa ya UNEP, kama taasisi isiyo na upendeleo kuhusiana na masuala ya mazingira inatokana na miaka 50 ya utafiti wa kisayansi wa kipekee unaongoza maamuzi na sera kuhusiana na mazingira.

Tangu kuanzishwa kwake katika mwaka wa 2005, tuzo la Mabingwa wa Dunia linalotolewa kila mwaka limetoa umaarufu na kusifia watu walio mstari mbele kupigania mazingira duniani, kuanzia kwa wanasayansi chupukizi, viongozi wa makampuni, maraisi hadi kwa mahamasishaji katika jamii.  Wao ni mfano wa watu wanaoweza kushawishi na wanaoweza kuigwa wanaonyesha kuwa juhudi za mtu mmoja au za kundi la watu zinaweza kuleta mabadiliko duniani.