Uongozi Unaozingatia Sera Award

Kitengo hiki cha tuzo hutuza watu binafsi au mashirika yanayoshugulikia umma ambayo juhudi na uongozi wake uwezesha kuleta mabadiliko makuu ndani na hata nje ya nchi. 

Washindi wa tuzo la Mabingwa wa Dunia huchaguliwa na waamuzi wa kimataifa kufuatia mapendekezo yanayotolewa na umma. Kiwango kikubwa cha mapendekezo yanayotolewa ni ishara ya ongezeko la idadi ya watu wanaoelewa ni nini kinachowezekana na wanaona kuwa kuna fursa ya kutunza na kuboresha mazingira.

Mabingwa wa Dunia ni sehemu ya watu wanaoweza kuigwa kutokana na juhudi zao mwafaka zilizoleta mabadiliko chanya ya kudumu kwa mazingira na kuboresha jamii zetu. Kupiga marufuku matumizi ya kemikali zinazodhuru ozoni, kuondoa risasi kwenye petroli, kukomesha matumizi ya plastiki inayotumika tu mara moja, utunzaji wa spishi zilizo hatarini kuangamia na ongezeko la matumizi ya nishati jadidifu ni ishara ya kujitolea kwa watu, juhudi zao, kushirikiana na uvumbuzi.