Mabingwa wa Dunia Mwaka wa 2021

Mabingwa wa Dunia Mwaka wa 2021 ni sehemu ya historia ya watu ambao juhudi zao zimefanikiwa kusababisha ushindi kwa mazingira ambao umebadilisha jamii zetu kuwa bora zaidi. Kukomeshwa kwa kemikali zinazoharibu ozoni, kuondolewa kwa madini ya risasi kutoka kwa petroli, kupiga marufuku matumizi ya plastiki inayotumika mara moja, kurejeshwa kwa viumbe vilivyotoweka katika eneo kwenye mifumo ya ekolojia iliyoboreshwa na kuongezeka kwa matumizi ya nishati jadidifu ni kutokana na kujitolea kwa watu, ushirikiano wao na uvumbuzi.