Kikao cha tano cha Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA) (UNEA-5) hutoa uongozi, kuchombea hatua za kimataifa za kushughulikia mazingira, na kuchangia utekelezaji wa Ajenda 2030 ya UN ya Maendeleo Endelevu na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yake.

Utangulizi

Wakati wa janga la COVID-19 na kutokana na kushauriana kwa kina na Nchi Wanachama na Wadau, kitengo cha utawala cha UNEA kiliamua tarehe 8 Octoba mwaka wa 2020 kuwa UNEA-5 iendeshwe kwa njia mbili. Kikao cha kwanza cha UNEA-5 kitaendeshwa mtandaoni tarehe 22 na tarehe 23 mwezi wa Februari 2021 na ajenda itakayoshughulikia masuala nyeti inayohitaji utaratibu wa kuyafanyia uamuzi. Masuala nyeti yanayohitaji majadiliano ya kina yataairishwa ili yashughulikiwe katika kikao cha ana kwa ana cha UNEA-5 kitakachofanyika mjini Nairobi katika mwezi wa Februari mwaka wa 2022.

Maandalizi ya kikao cha UNEA-5 kitakachoendeshwa mtandaoni yatafanyika wakati wamkutano wa tano wa Kamati ya Mabalozi wa Kudumu, utakaoendeshwa mtandaoni tarehe 15 na 16 February 2021.

Kaulimbiu:

Kaulimbiu ya UNEA-5 ni “Kuimarisha Juhudi za Kushughulikia Mazingira ili Kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu”.

Kaulimbiu hii inatoa wito wa kuimarisha juhudi za kushughulikia na kuboresha mazingira ili kufikia SDGs kupitia vipengele vyake vitatu vinavyoingiliana vya (kijamii, uchumi na mazingira). UNEA-5 hutoa kwa Nchi Wanachama na Wadau jukwaa la kushiriki na kutekeleza mikakati mwafaka inawezesha kutumizwa kwa vipengele vya mazingira vya Ajenda 2030 na SDGs, ikijumuisha malengo yanayohusiana na utokomeshaji wa umaskini na ruwaza endelevu ya matumizi na uzalishaji wa bidhaa. UNEA-5 pia inatoa fursa kwa Nchi Wanachama na Wadau kuchukua hatua kabambe za kujiimarisha na kutochafua mazingira kwa kuhakikisha kuwa uwekezaji kuimarisha uchumi baada ya janga la korona kutachangia maendeleo endelevu.

Rais wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa, kwa ushirikiano wa karibu na Utawala wa UNEA na Kamati ya Mabalozi wa Kudumu na Utawalawake, wataendelea kushirikiana kwa njia ya wazi na shirikishi ili kuhakakisha UNEA-5 iliyo na awamu mbili itafaulu.

Wasilana:

Tafadhali wasiliana na Sekritarieti ya UNEP unep-sgb@un.org ili kupokea taarifa zaidi.

Linki za Kurejelea:

Wawakilishi wa Nchi Wanachama wanaweza kupata stakabadhi kabla ya kikao, linki zinazohusiana na mkutano, linki za kurejelea na maelekezo kulia kwa ukrasa huu.