Kikao cha sita cha Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA-6) kitafanyika kuanzia tarehe 26 Februari hadi tarehe 1 Machi, mwaka wa 2024 katika makao makuu ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) jijini Nairobi, nchini Kenya. 

Kama chombo cha juu zaidi cha kufanya maamuzi duniani kuhusu mazingira, UNEA inalenga kusaidia kurejesha amani kati ya binadamu na mazingira, na kuboresha maisha ya watu walio hatarini zaidi duniani. 

UNEA-6 itaangazia jinsi ushirikiano wa nchi nyingi unavyoweza kusaidia kukabiliana na majanga ya aina tatu duniani; mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa mazingira na bayoanuai, na uchafuzi na taka. Ikiungwa mkono na sayansi dhabiti, utashi wa kisiasa na ushirikiano na jamii, Baraza hili litakuwa fursa kwa serikali duniani, mashirika ya uraia, jamii ya wanasayansi na sekta binafsi ya kuchagia sera ya kimataifa ya mazingira.

Kama jukwaa la pekee la wanachama kutika kote ulimwengu wa kushughulikia mazingira, UNEA hutoa jukwaa la kipekee la kufanyia maamuzi ya kijasiri na mawazo mapya ili kuweka mikakati mipya dhabiti ya kuwezesha hatua za pamoja za kushughulikia mazingira. Kwa kufanya hivyo, UNEA-6 itasaidia kufikiwa kwa malengo ya maendeleo endelevu.   

UNEA-6 itatanguliwa na mkutano wa Kamati ya Wawakilishi wa Kudumu ya kujadili mambo kwa mapana, ambayo itasaidia kuweka msingi wa kazi ya Baraza. 

Kuendeleza hatua tunazohitaji
Habari na matukio
WHEN:
26 Feb 2024 - 1 Mar 2024
WHERE:
Nairobi, Kenya

Pakua aouu rasmi ya UNEA

Pata atiba za vikao, matangazo, ramani na taarifa kwa wakati halisi popote ulipo. Pakua apu ya UNEA kwa kutumia kifaa kilichopo hapo chini.

Android

iOS