Kamati ya Wawakilishi wa Kudumu isiyofuata utaratibu maalumu

Kamati ya Wawakilishi wa Kudumu isiyofuata utaratibu maalumu (OECPR) ni taasis ya UNEA inayofanya kazi kwa kipindi maalum. OECPR hufanya kazi kama mkutano wa maandalizi ya ajenda ya UNEA na kujadili mapema na kuangazia yaliyomo na maneno ya kutumiwa katika maazimio yaliyopendekezwa, matamko na maamuzi ili kuunga mkono na kuidhinishwa na Baraza.Ikijumuisha wawakilishi wote walioidhinishwa kuwa sehemu ya Kamati ya Wawakilishi wa Kudumu, OECPR huandaa mikutano ya UNEA.  

Tangu kutokea kwa UNEA-3, mikutano ya OECPR imefanyika kwa kwa utaratibu wa kuhamishia wajibu mhusika wa kando pamoja na vikao vya UNEA ili kupunguza gharama na mikakati ya usafiri. OECPR ambazo zimefanyika ni pamoja na:

  • OECPR ya kwanza: Machi 24 hadi 28, 2014
  • OECPR ya pili: Februari 15 hadi 19, 2016 
  • OECPR ya tatu: Novemba 29 hadi 1 Desemba 1, 2017
  • OECPR ya nne: Machi 4 hadi 8, 2019
  • OECPR ya tano: Februari 15 hadi 19, 2021 
  • kikao cha 5 cha OECPR kilikuwa cha ana kwa ana: Februari 22 hadi 25, 2022   

Kwa mujibu wa aya ya 10 ya uamuzi wa 27/2 wa Baraza la Uongozi la wa tarehe 23 Februari mwaka wa 2013 na uamuzi wa 5/4 wa tarehe 2 mwezi wa Machi mwaka wa 2022, mkutano wa sita wa Kamati ya Wawakilishi wa Kudumu isiyofuata utaratibu maalumu utafanyika tarehe 19 hadi 23 Februari mwaka wa 2024. 

Mashauriano yasiyo rasmi katika mfumo wa vikundi vya kazi/makundi ya wasiliano yatakuwa kwa mfumo mseto wa mchanganyiko wa washiriki wa ana kwa ana na mtandaoni kupitia jukwaa la mtandaoni. Taarifa za ziada kuhusu ajenda na stakabadhi zitapatikana hivi karibuni. 

Soma zaidi kuhusu Kamati ya Wawakilishi wa Kudumu

Majukwaa ya Kikanda ya Mawaziri wa Mazingira  

Majukwaa ya Kikanda ya Mawaziri wa Mazingira ni nafasi nzuri kwa mazungumzo ya kisiasa na ushirikiano wa masuala ya mazingira katika ngazi za kikanda. Yanatumika kama jukwaa kwa Nchi Wanachama kuchangia mitazamo ya kikanda ya kikao kijacho cha UNEA. 

Majukwaa ya Kikanda ya Mawaziri wa  Mazingira hufanyika wakati wa kipindi cha vikao vya UNEA na huandaliwa na Ofisi za Kanda za UNEP.

Majukwaa ya Kikanda ya Mawaziri wa Mazingira mwaka wa 2023

Soma zaidi kuhusu Majukwaa ya Kikanda ya Mawaziri wa Mazingira mwaka wa Soma zaidi kuhusu

Tafadhali wasiliana na Sekretarieti ya UNEP kupitia unep-sgb@un.org kwa habari zaidi.

Mikutano ya Mashauriano ya Kikanda kati ya Makundi Makuu na Washikadau

Mikutano ya Mashauriano ya Kikanda  (RCM) hufanyika angalau mara moja katikati ya kipindi cha vikao vya UNEA na huandaliwa na Ofisi za Kanda za UNEP kwa ushirikiano wa karibu na Wasaidizi wa Kanda waliochaguliwa na Makundi Makuu.  Wakati wa mashauriano ya kikanda, misimamo ya pamoja huchukuliwa na changamoto zinazohusiana na kanda hujadiliwa.

Mikutano ya Mashauriano ya Kikanda kati ya Makundi Makuu na Washikadau mwaka wa 2023

Soma zaidi kuhusu Mikutano ya Mashauriano ya Kikanda

Michakato mingine ya maandalizi ya UNEA-6

Maandalizi ya Azimio la Mawaziri la UNEA-6

Mfululizo wa Rasimu za Tamko la Mawaziri zimesambazwa ili kupata maoni na mchangokutoka kwa Nchi Wanachama na Makundi Makuu na Washikadau. Rasimu na mchango wao vinaweza kupatikana kwenye ukurasa wa Maoni ya kujumuishwa kwa Tamko la Mawaziri.

Rasimu ya maazimio na maamuzi

Wajumbe wanaokusudia kuwasilisha rasimu ya maazimio na kuambatisha na maelezo ya dhana wanahimizwa kufanya hivyo kwa kutuma rasimu na maelezo zaidi kwa sekretarieti kufikia tarehe 11 Desemba mwaka 2023 ikiwezekana, na ifikapo tarehe 18 Desemba 2023 hivi karibuni, kulingana na  mwongozo kwa Nchi Wanachama kuhusu kuwasilisha rasimu ya maazimio na maamuzi kwa UNEA-6.

Maazimio na maamuzi yote yaliyowasilishwa yatapatikana mara moja kwenye Tovuti ya Maazimio ya UNEA -6 iliotengewa maazimio hayo. Tovuti ya maazimio ni tovuti ina nenosiri maalum ambayo itajumuisha taarifa zote muhimu ikiwa ni pamoja na rasimu ya azimio na muhtasari wa dhana, sehemu kuu ya mtetezi wa azimio hilo, wafadhili-wenza, makala kuhusu usuli, maelezo ya kiufundi ya sekretarieti, na matoleo mbalimbaliya rasimu kama zinavyobadilika mashauriano na majadaliano yanapoendelea.

WHEN:
26 Feb 2024 - 1 Mar 2024
WHERE:
Nairobi, Kenya

Pakua aouu rasmi ya UNEA

Pata atiba za vikao, matangazo, ramani na taarifa kwa wakati halisi popote ulipo. Pakua apu ya UNEA kwa kutumia kifaa kilichopo hapo chini.

Android

iOS