Hafla rasmi za kando za UNEA-6

 

Orodha ya hafla rasmi za kando (PDF)

 

Hafla rasmi za kando zitafanyika ana kwa ana au kupitia mtandaoni kwa kipindi cha siku tano za kikao cha sita cha Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA-6), wakati wa mapumziko ya chakula cha mchana na jioni.  Jumla ya nafasi 16 zimetengwa kwa hafla za ana kwa ana na nafasi nyingine 17 kwa hafla za kando kupitia mtandaoni.

Kila mojawapo wa hafla hizi za kando za dakika 75 zinanuiwa kuimarisha na kukamilishana na kikao cha UNEA-6 kwa kutoa fursa ya kipekee ya kujadili kaulimbiu, kubadilishana mawazo, kutafuta masuluhisho na kuchochea ushirikiano wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa bayoanuai na uchafuzi.  

Wito wa kutuma maombi ulifungwa tarehe 17 Novemba mwaka wa 2023.

Kwa maswali kuhusu hafla rasmi za kando, tafadhali wasiliana kupitiaunea-side-events@un.org  ukionyesha [Jina la Hafla ya Kando] na shirika kuu linaloandaa katika mada ya barua pepe. 

LOADING...

WHEN:
26 Feb 2024 - 1 Mar 2024
WHERE:
Nairobi, Kenya

Pakua aouu rasmi ya UNEA

Pata atiba za vikao, matangazo, ramani na taarifa kwa wakati halisi popote ulipo. Pakua apu ya UNEA kwa kutumia kifaa kilichopo hapo chini.

Android

iOS